Pata taarifa kuu

Haiti: Waziri Mkuu Ariel Henry avunja ukimya wake baada ya wiki ya ghasia

Baada ya wiki ya maandamano, ghasia na visa vya uporaji mkubwa nchini Haiti, kaimu waziri mkuu hatimaye amevunja ukimya wake. Jioni ya Jumapili, Septemba 18, Ariel Henry alitoa hotuba kwenye televisheni. Lakini wale waliotarajia mkuu wa serikali kubadili uamuzi wake wenye utata wa kupandisha bei ya mafuta kwa kasi walikatishwa tamaa.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ametaka vizuizi hivyo kuondolewa baada ya wiki moja ya ghasia. Hapa, ni Julai 20, 2021 huko Port-au-Prince.
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ametaka vizuizi hivyo kuondolewa baada ya wiki moja ya ghasia. Hapa, ni Julai 20, 2021 huko Port-au-Prince. AP - Joseph Odelyn
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki ya machafuko nchini Haiti, hatimaye Waziri Mkuu alihutubia raia wake. “Kutokana na mabadiliko ya hali hiyo, nawaomba wote watulie. Pamoja tunaweza kutatua matatizo yote. Naelewa kwanini wanaghadhabishwa. Nataka kuwaambia wale ambao wamepoteza mali zao ambao wamechukua maisha yao yote kujenga: Ninajiunga nao kwa uchungu wanaoupata, "alisema.

Ariel Henry alisema maandamano, visa vya uporaji na vurugu za siku za hivi karibuni hazina uhusiano wowote na hasira ya raia, lakini vurugu hizo zimepangwa na zinafadhiliwa. "Tumechukua hatua kadhaa zinazohusu desturi za Haiti. Hatua hizi zinapaswa kuiwezesha Serikali kudhibiti vyema kile kinachoingia nchini, kupunguza ulanguzi wa silaha na dawa za kulevya na kuongeza mapato. Lakini kuna watu ambao hawafurahii sana hatua hizi. Hao ndio wanachochea maandamano na vurugu hizi. Iwe wako Haiti au nje ya nchi, tumeshawabaini,” alisema.

Wito wa kuondoa vizuizi

Waziri Mkuu amewaomba wananchi kuwasaidia polisi kuondoa vizuizi vinavyozuia barabara kuu nchini kote. "Serikali iinafanya kazi siku nzima kufungua barabara kuu ili maisha yarudi kuwa ya kawaida. Msaada wenu kwenu nyote ni muhimu. Ondoweni vizuizi barabarani katika vitongoji vyenu vyote na mzuie wengine kuweka tena vizuizi!, ameongeza. Kwa sababu wanawake wajawazito wanapaswa kwenda hospitali, wagonjwa wanahitaji kwenda kutibiwa, wafanyabiashara wanapaswa kuuza bidhaa zao mitaani. Na magari lazima yawe na uwezo wa kutumia barabara kusambaza mafuta katika mikoa yote ya nchi”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.