Pata taarifa kuu
UCHAGUZI WA URAIS

Wabrazil wapiga kura katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkubwa

Wabrazili wapatao milioni 156 wameitwa Jumapili hii, Oktoba 2 kupiga kura katika nchi hiyo kubwa zaidi katika Amerika ya Kusini ili kuchagua rais wao kwa kipindi cha miaka minne ijayo. 

Sehemu ya kupigia kura katika kituo cha kupigia kura huko São Pedro; jamii kwenye Mto Amazonas, Oktoba 1, 2022.
Sehemu ya kupigia kura katika kituo cha kupigia kura huko São Pedro; jamii kwenye Mto Amazonas, Oktoba 1, 2022. © Bruno Kelly / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais anayemaliza muda wake Jair Bolsonaro anapewa nafasi ya kushindwa dhidi ya mpinzani wake, Luiz Inacio Lula da Silva aliye kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2003 hadi 2010. 

Lula da Silva wa mrengo wa kushoto, aliyehukumiwa jela na kisha kuachiliwa miaka miwili baadaye, tayari anaamini ushindi wake katika moja ya chaguzi zenye ushindani mkubwa nchini.

Wagombea hao wawili wakuu walifanya jkampeni zao huko São Paulo, mji mkuu wa kiuchumi, siku moja kabla ya uchaguzi.

Jumamosi Oktoba 1, Lula alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo tayari alijionyesha kama rais mtarajiwa: aliahidi kuiondoa nchi katika mgogoro wa kiuchumi na kijamii. Lakini yeye, wakati huo, alipunguza matarajio kwa kusema kwamba bila shaka itachukua muda.

Lula anajua ana kila nafasi ya kushinda uchaguzi, lakini anataka kabisa kushinda katika duru ya kwanza. Iwapo atapita na zaidi ya 50% ya kura, itakuwa vigumu kwa Jair Bolsonaro kupinga uchaguzi, anaripoti mwandishi wetu maalum huko São Paulo, Achim Lippold.

Kulingana na kura za hivi punde zilizochapishwa Jumamosi jioni, Lula anaweza kushinda kura nyingi leo, lakini inaweza kuwa chini ya kura chache: taasisi za upigaji kura zinampa Lula 50% au 51% ya kura, na kuongoza pointi 14 dhidi ya Jair Bolsonaro, anaripoti mwandishi wetu huko São Paulo, Martin Bernard.

Kando na wagombea wakuu hao wawili, kuna wagombea wengine 10 wanaowania duru ya kwanza. Kwa hivyo Lula anatumai kunufaika kutokana na uhamisho wa kura, endapo kutakuwa na duru ya pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.