Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Kampeni za uchaguzi wa urais zaanza Brazil

Huu ni mwanzo rasmi wa kampeni za uchaguzi nchini Brazil.  Lula da Silva na Jair Bolsonaro, ni miongozi mwa wagombea zaidi ya kumi ambao wanaowania katika kiti cha urais nchini Brazil. 

Rais aliye madarakani kutoka mrengo mkali wa kulia, Jair Bolsonaro, na shujaa wa mrengo wa kushoto, Lula, ndio wagombea wawili wa katika uchaguzi wa urais wanaopewa nafasi kubwa ya mmoja wao kushinda uchaguzi huo, nchini Brazil.
Rais aliye madarakani kutoka mrengo mkali wa kulia, Jair Bolsonaro, na shujaa wa mrengo wa kushoto, Lula, ndio wagombea wawili wa katika uchaguzi wa urais wanaopewa nafasi kubwa ya mmoja wao kushinda uchaguzi huo, nchini Brazil. © Fotomontagem RFI/Adriana de Freitas/AP photos
Matangazo ya kibiashara

Lula da Silva na Jair Bolsonaro ambao wanaonekana kuwa na wafuasi wengi wamekuwa wakizunguka nchi nzima kwa wiki kadhaa ili kukukutana na wapiga kura, lakini kampeni rasmi, ikiwa ni pamoja na mikutano na usambazaji wa vipeperushi, imeidhinishwa tu kuanzia Jumanne hii, Agosti 16. Matangazo ya TV kuhusiana na kampeni hizi yataonyeshwa tu kuanzia Agosti 26.

Jair Bolsonaro amechagua kurudi katika mji mdogo wa Juiz de Fora ili kuzindua kampeni yake rasmi. Rais anayemaliza muda wake kutoka mrengo wa kulia, Jair Bolsonaro atatoa hotuba yake kwenye jukwaa lililowekwa kwenye njia panda ambapo alichomwa kisu na mtu aliyekuwa na ugonjwa wa katika umati wa watu, Septemba 6, 2018.

Kapteni huyu wa zamani wa jeshi asiyependa udikteta wa kijeshi, ambaye sasa ana umri wa miaka 67, amezidisha upinzani dhidi ya taasisi, hasa Mahakama ya Juu. Akidharau vyombo vya habari vya kawaida, alijizuia na njia za kawaida za mawasiliano, akipendelea kuzungumza moja kwa moja na mamilioni ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii, ambayo yeye ni mtumiaji mwenye shauku.

Lula anarudi kutoka mbali

Kuhusu Lula da Silva, amejiunga na chama cha wafanyakazi wa chuma, ambapo alianza kazi yake ya kisiasa katika viunga vya São Paulo. Shujaa wa mrengo wa kushoto na mwanzilishi wa chama cha PT ametoka mbali. Lula da Silva ambaye alihukumiwa kwa ufisadi mwaka wa 2017, kufungwa mwaka mmoja na nusu, alikataliwa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2018, aliachiliwa huru mwezi Machi 2021 baada ya Mahakama ya Juu kufuta adhabu yake. Mwishoni mwa mwezi Aprili 2022, Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilihitimisha kwamba uchunguzi na kufunguliwa mashtaka kwa Lula kulikiuka haki yake ya kuhukumiwa na mahakama isiyopendelea upande wowote.

Baada ya kurejeshewa haki zake za kisiasa, kiongozi huyu - ambaye wengi walidhani kuwa amemalizwa kisiasa - atawania kwenye kiti cha urais, miaka kumi na miwili baada ya kuondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.