Pata taarifa kuu

Brazil: Ukosoaji na uchochezi wakumba mahojiano ya kwanza ya kampeni ya Jair Bolsonaro

Rais wa Brazil amefanya mahojiano yake ya kwanza ya televisheni kama sehemu ya kampeni ya uchaguzi wa urais. Jumatatu jioni, Jair Bolsonaro, anayewania tena kiti chake cha urais, alikuwa wa kwanza kuzindua mzunguko huu wa mahojiano kwenye kituo cha Globo, ambacho kinawahoji wiki hii wagombea wanne wanaotabiriwa kuwa na kura nyingi kura wanawasilisha.

Katikati ya kampeni za urais, rais wa Brazil alitoa mahojiano yake ya kwanza kwenye kituo cha Globo.
Katikati ya kampeni za urais, rais wa Brazil alitoa mahojiano yake ya kwanza kwenye kituo cha Globo. AFP - MARCOS SERRA
Matangazo ya kibiashara

Mahojiano haya ni ya kwanza kwa Jair Bolsonaro, ambaye wakati wa uchaguzi uliopita hakushiriki mdahalo wowote au mahojiano ya televisheni, baada ya kudungwa kisu wakati wa kampeni.

Maandamano ya watu waliokuwa wakibebelea sufuria yalianza saa 8:30 usiku, pamoja na mahojiano ya rais wa Brazil, waandamanaji wakimtaka rais ajiuzulu 'fora Bolsonaro' .

“Mimi hushambuliwa kila mara na jaji wa Mahakama ya Juu Zaidi,” amesema. Wakati wa mahojiano, Jair Bolsonaro pia amekanusha kuwatusi majaji wa Mahakama ya Juu na mahakama ya uchaguzi.

Pia amekanusha kuzuia kandarasi za chanjo wakati wa janga la Uviko-19. Hatimaye, amerejelea hoja zake akihoji kutegemewa kwa masanduku ya kura ya kielektroniki.

Pia kuna sentensi hii ya uchochezi: "Mnanihimiza kuwa dikteta", amesema rais wa Brazil kwa mwandishi wa habari William Bonner, ambaye alimhoji juu ya ukaribu wake na kituo hicho, ambacho Jair Bolsonaro alitumia kukikosoa kabla ya kutawala.

Licha ya ukosoaji wa mara kwa mara wa rais kwenye kituo cha Globo, na ukweli wa kuwakatisha tamaa wafuasi wake kuhudhuria.

Katika wiki za hivi karibuni, kura zinakaribiana katika uchaguzi kati ya rais na mpinzani wake mkuu, Lula. Rais huyo wa zamani atahojiwa siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.