Pata taarifa kuu
CANADA-SIASA

Canada: Trudeau kuitisha uchaguzi wa mapema Septemba 20

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau anaazimia kuitisha uchaguzi wa mapema wa bunge mnamo Septemba 20 na anatarajia kutangaza uamuzi wake Jumapili, kulingana na vyanzo vinne vilivyo karibu na mpango, vilivyonukuliwa na shirika la habari la REUTERS.

Ili kuzindua rasmi mchakato wa uchaguzi, Justin Trudeau atalazimika kukutana na kiongozi Mkuu wa Canada, Mary Simon, mwakilishi rasmi wa Malkia Elizabeth, Mkuu wa Nchi, kumuomba avunje Bunge
Ili kuzindua rasmi mchakato wa uchaguzi, Justin Trudeau atalazimika kukutana na kiongozi Mkuu wa Canada, Mary Simon, mwakilishi rasmi wa Malkia Elizabeth, Mkuu wa Nchi, kumuomba avunje Bunge Dave Chan AFP
Matangazo ya kibiashara

Washauri wa Justin Trudeau wamekuwa wakizungumza kwa miezi kadhaa juu ya uwezekano wa uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka huu, miaka miwili kabla ya kumalizika kwa muhula wa bunge la sasa.

Serikali ya Canada ina viti vichache katika Bunge, hali ambayo inaifanya kutegemea vyama vya upinzani kupitisha miswada yake.

Chama cha Justin Trudeau kinaweza kutarajia kunufaika, ikiwa kuna uchaguzi mwezi ujao, kutokana na kufufuliwa tena kwa uchumi wa Canada baada ya janga la Corona na maendeleo ya kampeni ya chanjo ya COVID-19.

Ili kuzindua rasmi mchakato wa uchaguzi, Justin Trudeau atalazimika kukutana na kiongozi Mkuu wa Canada, Mary Simon, mwakilishi rasmi wa Malkia Elizabeth, Mkuu wa Nchi, kumuomba avunje Bunge.

Mahojiano haya yamepangwa kufanyika Jumapili asubuhi, Agosti 15, vimesema vyanzo hivo, ambavyo havikutaka kutajwa majina.

Wataalam kadhaa wa katiba wanabaini kwamba Mary Simon hapaswi kupinga ombi la Justin Trudeau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.