Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTUMWA-USALAMA

Mvutano waibuka kati ya Trump na Pelosi kuhusu alama za enzi za utumwa

Rais Donald Trump amesema hakubailiani na fikra yoyote ya kubadilisha majina ya kambi za kijeshi zilizotajwa baada ya majenerali walioongoza jeshi la Marekani na kubaini kwamba huo ni utovu wa nidhamu kwa wanajeshi.

Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mazungumzo na viongozi wa jamii ya Wamarekani weusi katika Ikulu ya White House, Juni 1 hadi 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mazungumzo na viongozi wa jamii ya Wamarekani weusi katika Ikulu ya White House, Juni 1 hadi 2020. SAUL LOEB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Twitter, unakuja wakati huu ambapo maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi, yaliyosababishwa na kifo cha George Floyd aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi , yameibua mjadala mkubwa kuhusu enzi za utumwa katika nchi hiyo inayoundwa na jamii za watu mbalimbali.

Kambi kumi za jeshi, zinazopatikana Kusini mwa Marekani, zote zimepewa majina ya majenerali wa zamani kutoka Kusini mwa nchi hiyo waliohusika katika kutukuza utumwa.

Jumanne wiki hii, Waziri wa Ulinzi , kupitia msemaji wa wizara yake, amesema " yuko tayari kwa mazungumzo juu ya mada hiyo". Lakini katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Donald Trump alibaini kwamba kambi hizo za jeshi za "kihistoria" ni sehemu ya urithi wa Marekani. Na kusisitiza kwamba serikali yake "haina nia yoyote" ya kujadili uwezekano wa kubadilisha majina ya kambi hizo. "Mnapaswa kuheshimu jeshi letu! ", amesema rais wa Marekani.

Matamshi hayo ya bwana Trump yanajiri kufuatia ripoti kwamba maafisa wakuu wa jeshi walikuwa tayari kuruhusu mabadiliko kufuatia maandamano yaliosababishwa na kifo cha George Floyd.

Kwa wengi, alama za mataifa ya kusini yaliokuwa yakiwahifadhi watumwa ambayo baadaye yalijiondoa katika biashara hiyo na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe Marekani - zilikuwa na kumbukumbu za kibaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.