Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Maelfu wakusanyika mbele ya mwili wa George Floyd kabla ya mazishi

Wiki mbili baada ya kifo chake huko Minneapolis, kilishosababishwa na afisa wa polisi, mwili wa George Floyd umerejeshwa huko Houston kwa ajili ya mazishi Jumanne, Juni 9.

Maelfu ya watu walipishana mbele ya jeneza la George Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho.
Maelfu ya watu walipishana mbele ya jeneza la George Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Waombolezaji wengi walitengeneza ishara ya msalaba wakati wakikaribia jeneza la Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho wakati wengine wakipiga magoti au kuinamisha vichwa na kumuombea kimyakimya mtu ambaye amekuwa ishara ya karibuni ya vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Marekani.

Hafla hiyo ilikuwa ya mwisho katika msururu wa hafla zilizoandaliwa za kumuaga Floyd. Atazikwa leo katika mazishi ya faragha kando ya kaburi la mamake mjini Houston, ambako ndiko alikokulia.

Mjini Washington, wajumbe wa Democratic walipiga magoti na kusalia kimya kwa dakika nane na sekunde 46, muda alioutumia polisi mweupe kugandamiza shingo ya Floyd akitumia goti.

Jumatatu, watu waliruhusiwa kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Marekani huyo mweusi aliyefariki dunia mikononi mwa polisi.

Karibu watu 7,000 walikuja kumuaga George Floyd Kusini mwa jiji la Houston Jumatatu wiki hii.

Kifo cha George Floyd, ni ishara tosha ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani na kwingineko ulimwenguni alisema binamu yake Shareeduh Tate wakati wa ibada ya kuaga mwili wake huko Minneapolis wiki iliyopita.

George Floyd anazikwa Jumanne wiki hii huko Houston, jiji ambalo alikulia na kwa muda mrefu alikuwa ni mtu mkarimu kwa wakazi wa mji na mcheshi kwa kila mtu, watu walioishi pamoja wamesema.

Kifo cha George Floyd kilizusha maandamano makubwa katika miji mbalimbali nchini Marekani na nje ya nchi hiyo, hususan barani Ulaya.

Mama yake alihamia Houston mara tu baada ya kuzaliwa George Floyd huko North Carolina mwaka 1973. Alilelewa katika eneo la "Third Ward", kitongoji cha watu weusi na maskini kinachopatikana katikati mwa jiji kubwa la Texas.

Derek Chauvin, polisi mweupe aliyeonekana kwenye video akigandamiza shingo ya Floyd kwa kutumia goti wakati akiwa amefungwa pingu, kwa karibu dakika tisa, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii. Anakabiliwa na kifungo cha miaka hadi arobaini kwa kosa la kuuwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.