Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Marekani: Ndugu wa George Floyd atoa wito kwa mageuzi ya polisi

Baada ya mazishi ya Mmarekani mweusi ambaye kifo chake kilisababisha maandamano makubwa nchini Marekani, wabunge wanafikiria kufanya marekebisho ya idara ya polisi.

Philonise Floyd, ndugu wa George Floyd, akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya sheria ya Baraza la Wawakilishi huko Washington Juni 10, 2020.
Philonise Floyd, ndugu wa George Floyd, akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya sheria ya Baraza la Wawakilishi huko Washington Juni 10, 2020. POOL / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / GETTY IMAGES VIA AFP
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya sheria ya Baraza la Wawakilishi imewaitisha baadhi ya mashahidi ili kusaidia muswada wa sheria uliowasilishwa bungeni na wabunge wa chama cha Democratic. Mtu wa kwanza miongoni mwa mashahidi ambao walisikilizwa na kamati hiyo ni Philonise Floyd, kaka wa George Floyd.

"Taifa linataka na linastahili mabadiliko makubwa," ametangaza Jerrold Nadler, akifungua kikao cha kamati ya sheria ya Baraza la Wawakilishi.

Wabunge kutoka chama cha Democratic wanakusudia kurekebisha mfumo mzima wa idara ya polisi nchini Marekani: tayari wamewasilisha muswada wa sheria. Na ili kuunga mkono hoja yao, walimwitisha kaka wa Georges Floyd.

"Labda ninapoongea na nyinyi leo, naweza kuhakikisha kuwa hakufa kwa sababu zisizoeleweka," Philonise Floyd amesema.

"Siku zote georges alijitolea kwa ajili ya familia yetu, na alijitolea kwa watu wengine asiyowafahamu. Alikuwa mtu muhimu katika jamii. Kwenye video ya mauaji yake, alimwita afisa wa polisi aliyesababiosha kifo chake "bwana" akimuonesha kuwa maisha yake yako hatarini, " Philonise Floyd ameongeza.

"Siwezi kuwaambia ni maumivu gani ninayoyahisi ninapoona kitu kama hiki. Unapomtazama kaka yako mkubwa unayempenda sana anapofariki! Anafariki akimwita mama yake! Nimechoka na maamivu haya! Niko hapa kuomba mkomeshe ukatili huu!

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amewashutumu wabunge kutoka chama cha Democratic kutaka kusambua idara ya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.