Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Marekani: Mmoja wa maafisa wa polisi aliyehusika na kifo cha George Floyd aachiliwa kwa dhamana

Thomas Lane, mmoja wa maafisa wanne wa polisi wa Minneapolis aliyehusika na kukamatwa kwa George Floyd Mei 25, amechiliwa kwa dhamana Jumatano wiki hii.

Maafisa wa Polisi wa Minneapolis wakati wa maandamano baada ya kifo cha George Floyd, Juni 7, 2020.
Maafisa wa Polisi wa Minneapolis wakati wa maandamano baada ya kifo cha George Floyd, Juni 7, 2020. Kerem Yucel / AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi huyo, aliyefukuzwa kazini kama maafisa wengine watatu waliohusika na kifo cha Marekani huyo mweusi, aliondoka gerezani kaunti ya Hennepin.

Thomas Lane alitakiwa kulipa dhamana ya dola 750,000, shirika la habari la Reuters limeripoti. Wakili wake, Earl Grey, ameliambia Gazeti la kila siku la Star-Tribune, huko Minneapolis, kwamba watu walijitolea kuchangia kwa dhamana hiyo ili mteja wake aweze kuachiliwa.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amewashutumu wabunge kutoka chama cha Democratic kutaka kusambua idara ya polisi.

Jumatano wiki hii Kamati ya sheria ya Baraza la Wawakilishi iliwaitisha baadhi ya mashahidi ili kusaidia muswada wa sheria uliowasilishwa bungeni na wabunge wa chama cha Democratic. Mtu wa kwanza miongoni mwa mashahidi ambao walisikilizwa na kamati hiyo ni Philonise Floyd, kaka wa George Floyd, ambaye amesema:"Siwezi kuwaambia ni maumivu gani ninayoyahisi ninapoona kitu kama hiki. Unapomtazama kaka yako mkubwa unayempenda sana anapofariki! Anafariki akimwita mama yake! Nimechoka na maamivu haya! Niko hapa kuomba mkomeshe ukatili huu!”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.