Pata taarifa kuu
MAREKANI-UHAMIAJI-USALAMA

Mamia ya wahamiaji wakamatwa Mississippi

Polisi nchini Marekani imeendesha operesheni kabambe na kuwakamata wahamiaji 700 wasiokuwa na vibali halali katika mji Mississippi, kusini mwa nchi hiyo.

Watu hawa wanatuhumiwa kuwa wahamiaji haramu. Walikamatwa Agosti 7, 2019 katika mfululizo wa operesheni katika jimbo la Mississippi.
Watu hawa wanatuhumiwa kuwa wahamiaji haramu. Walikamatwa Agosti 7, 2019 katika mfululizo wa operesheni katika jimbo la Mississippi. HO / US Immigration and Customs Enforcement / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sera ya uhamiaji ya Donald Trump inaendelea kuzua utata nchini Marekani. Wakati rais wa Marekani alikuwa ziarani Jumatano, Agosti 7 katika miji ya Texas na Ohio ili kuwafariji waathiriwa wa mauaji ya mwishoni mwa wiki iliyopita, polisi wa uhamiaji waliendesha operesheni kabambe katika historia ya nchi hiyo. Karibu watu 700 walikamatwa, huku watoto kadhaa wakitelekezwa.

Polisi iliendesha operesheni hiyo katika miji mitano ya Mississipi. Maafisa 600 wa polisi walilenga viwanda saba.

Mwendesha mashtaka wa umma amesema watu 680 wamekamatwa baada ya uvamizi uliofanywa katika viwanda vinavyotengeza chakula.

Kiasi kikubwa cha waliokamatwa ni raia wa Amerika ya Kusini.

Maafisa wa uhamiaji nchini humo wanasema huenda ikawa hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya wahamiaji kukamatwa katika jimbo moja la Marekani.

Mapambano dhidi ya wahamiaji haramu ni mojawapo ya ahadi kuu alizotoa Rais Donald Trump wakati alipokuwa anachukua mamlaka.

Polisi walifika saa 2 asubuhi, wakizingira majengo hayo ili kuzuia wafanyakazi kutoka. Jumla watu 680, wengi wao wakiwa wenye asili ya Uhispania walikamatwa.

Wale ambao waliweza kudhihirisha kuwa wanaishi nchini Marekani kwa njia ya kisheria wameachiliwa, lakini kuna mamia wengine ambao bado wanashikiliwa.

Jumatano ilikuwa siku ya kwanza ya shule, na visomo vilipomalizika, watoto wengi walijikuta wakiwa peke yao ... Wale waliopata bahati walipelekwa na majirani zao, lakini wengi walipewa hifadhi katika maeneo wanakofanya mazoezi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.