Pata taarifa kuu
MAREKANI-WAHAMIAJI-USALAMA

Mkuu wa polisi wa mipaka ajiuzulu nchini Marekani

Mkuu wa polisi ya mipaka nchini Marekani, John Sanders, ametangaza kuachia ngazi baada ya kugundulika kwamba watoto wahamiaji wanazuiliwa katika mazingira mabaya, hali ambayo ilifichuliwa kwa vyombo vya habari.

Mkuu wa polisi ya mipaka Marekani, John Sanders, ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake ifikapo Julai 5.
Mkuu wa polisi ya mipaka Marekani, John Sanders, ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake ifikapo Julai 5. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe kwa maafisa wake, Kaimu Mkuu wa polisi wa mipaka nchini Marekani John Sanders ametangaza kwamba atajiuzulu kwenye nafasi yake Julai 5.

Tangazo la kujiuzulu kwake linakuja siku chache baada ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Human Right Watch kuchapisha ripoti mbaya kuhusu hali ya watoto 250 waliotengwa na familia zao wanazuiliwa katika kituo cha Clint, karibu na El Paso, huko Texas.

"Watoto walipofika kwenye chumba cha mkutano, hatukuamini macho yetu," Warren Binford, mmoja wa wanasheria waliokutana na watoto hao, amesema katika mahojiano na kituo cha MSNB.

Walikuwa wagonjwa, walipungua kimwili, walikuwa wachafu sana, na haraka walianza kutuzungumzia kuhusu jinsi wanavyohisi njaa.

"Walieleza madhila mbalimbali yanayowakumba tangu kuzuiliwa katika kituo hicho, amesema Warren Binford.

"Ushuhuda wa wanasheria umezua hisia mbalimbali nchini. Siku ya Jumatatu usiku watoto walihamishwa, lakini Jumanne hii wiki hii, watoto mia moja walilazimishwa kurudi kwenye kituo hicho, kwa kukosa nafasi mahali pengine, amearifu mwandishi wetu huko Washington, Anne Corpet.

Alipoulizwa kuhusu mazingira ambamo wanazuiliwa watotohao, rais wa Marekani Donald Trump amesema "ana na wasiwasi sana" akibaini kwamba hali hiyo ni "bora zaidi kuliko ile iliyo kuwa chini ya utawala wa Obama".

"Tunasubiri wenzetu kutoka chama cha Democratic kukubali kutoa misaada ya kibinadamu. Labda watakubali kuhusu msaada huu wa kibinadamu, "ameongeza rais wa Marekani.

Wabunge kutoka chama cha Democratic wamekubali kutoa dola bilioni 4.5 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa wahamiaji kwenye mpaka. Lakini hawaamini kwamba wenzao kutoka chama cha Republican, ambao ni wengi katika bunge la Seneti, watapitisha nakala hiyo: wanataka sehemu ya bajeti hiyo ipewe polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.