Pata taarifa kuu
MAREKANI-HOUSTON- HALI YA HEWA

Wataalam waonya kurejea kwa kimbunga Harvey Houston

Waokoaji nchini Marekani wakiwa kwenye boti, malori na helicopter wameendelea kukabiliana na athari za kimbunga Harvey kilichoikumba pwani ya jimbo la Texas na Houston, wakati huu wataalamu wakionya kuhusu uwezekano wa kurejea kwa kimbunga hicho kwa mara ya pili.

Houston yakumbwa na mafurikokufuatia kimbunga Harvey, Agost 27, 2017.
Houston yakumbwa na mafurikokufuatia kimbunga Harvey, Agost 27, 2017. REUTERS/Richard Carson
Matangazo ya kibiashara

Rais wa nchi hiyo Donald Trump ameahidi serikali kuwasaidia wananchi wa maeneo yaliyoathirika na mafuriko na kukiri kuwa hali ni mbaya zaidi kwenye baadhi ya maeneo.

Maofisa wa serikali wamesema licha ya juhudi kubwa zilizofanyika, bado kuna maelfu ya raia wamenaswa kwenye nyumba zao na baadhi ya maeneo yamefurika mamia ya watu wanaohitaji msaada.

Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga cha Harvey yameuacha mji wa Houston ambao ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Marekani katika hali mbaya huku uwanja wake wa ndege na barabara kuu vikilazimika kufungwa huku mamia ya makazi ya raia yakijaa maji.

Viwanja viwili vya ndege kwenye mji huo vilifungwa huku hospitali muhimu nazo zikilazimika kuwahamisha wagonjwa, katika mafuriko ambayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu watatu.

Awali kitengo cha maafa nchini Marekani kilisema mafuriko haya hayajawahi kushuhudiwa katika historia za vimbunga vilivyoikumba nchi hiyo. Watu zaidi ya watu elf mbili wameokolewa.

Maelfu ya raia wameokolewa huku watalaamu wakionya kuwa mafuriko zaidi yanatarajiwa.

Watu wawili walipoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika jimbo laTexas kufuatia Kimbunga Harvey, ambacho kimekua sasa dhoruba ya kitropiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.