Pata taarifa kuu
MAREKANI-HALI YA HEWA

Kimbunga Harvey chasababisha uchumi wa Texas kuanguka

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika jimbo laTexas kufuatia Kimbunga Harvey, ambacho kimekua sasa dhoruba ya kitropiki.

Kimbunga Harvey chasababisha uharibifu mkubwa kama hapa kwenye ghala la mafuta katika mji wa Seadrift, Texas, Agosti 26, 2017.
Kimbunga Harvey chasababisha uharibifu mkubwa kama hapa kwenye ghala la mafuta katika mji wa Seadrift, Texas, Agosti 26, 2017. REUTERS/Rick Wilking
Matangazo ya kibiashara

Upepo wenye kasi ya kilomita 215 kwa saa ulipiga pwani kadhaa siku ya Jumamosi, wakazi wengi walikimbilia kwenye mahandani na mafuriko makubwa yaanatarajiwa siku zijazo. Athari za kiuchumi pia zinaweza kuwa kubwa.

Kwa tahadhari, robo ya vifaa vua mafuta katika Ghuba ya Mexico vimefungwa kabla ya kupita kwa kimbunga hiki. Kiwango cha uharibifu hakijaijulikana bado, lakini Mamlaka ya Dharura nchini Marekani imebaini kwamba itachukua miaka kadhaa kwa kufuta athari za janga hili.

Texas, ambayo imekumbwa na kimbunga Harveyi ni, baada ya California, jimbo la pili lenye nguvu zaidi nchini Marekani katika masuala ya kiuchumi. Jimbo hili lingelikua huru, uchumi wake ungekuwa katika kiwango cha kile cha Uhispania au Canada.

Texas huzalisha asilimia 20 ya mafuta ya ya Marekani na 30% ya gesi asilia. Pia ni jimbo la pili kwa kilimo, hasa kwa mifugo na pamba. Kiwango cha ukosefu wa ajira kiko chini ya wastani wa kitaifa.

Na, kwa miaka 30 Texas ilipanda kiuchumi. Imekuwa kitovu muhimu kwa maendeleo ya teknolojia mpya, umeme, programu ya bioteknolojia na ujenzi wa viwanja vya ndege. Texas inatoa 10% ya uzalishaji wa umeme na 10% ya uzalishaji wa saruji na matofali.

Wakati huo huo watu takriban 2,000 wameokolewa kutoka kwa mafuriko katika mji wa Houston na viunga vyake, huku kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa sana maeneo ya jimbo la Texas.

Kumekuwa na ripoti za kutokea kwa vifo pamoja na magari kadhaa kuzidiwa na nguvu za maji.

Hata hivyo, uchunguzi bado unaendelea, afisi ya liwali mkuu wa wilaya ya Harris, Darryl Coleman imesema.

Ndege iliyoharibiwa na kimbunga Harvey kwenye uwanja wa ndege karibu na Fulton, Texas, Agosti 26, 2017.
Ndege iliyoharibiwa na kimbunga Harvey kwenye uwanja wa ndege karibu na Fulton, Texas, Agosti 26, 2017. REUTERS/Rick Wilking

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.