Pata taarifa kuu
MAREKANI

Kimbunga Harvey chapiga Texas Marekani

Kimbunga Harvey kimesababisha maporomoko ya ardhi katika Ghuba ya pwani ya Texas jana Ijumaa, wataalamu wa hali ya hewa wamesema na kuonya kuwa mafuriko ya maafa yanatarajiwa kutokana na kuanza kwa mvua kubwa zinazo ambatana na dhoruba kali.

Taa zikiwa zimeng'olewa na kimbunga Harvey
Taa zikiwa zimeng'olewa na kimbunga Harvey REUTERS/Adrees Latif
Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amemtaka gavana wa wilaya ya Texas Greg Abbott kutangaza janga kuu katika eneo hilo ili kuharakisha misaada ya shirikisho kwa mamilioni ya watu ili kuwaondoa hatarini.

Kimbunga hicho ni kikali kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani kwa takribani miaka 12 .

Hili ni janga kubwa na la kwanza tangu rais Donald Trump aingie madarakani huku akitarajiwa kuelekea katika eneo lililoathirika mapema juma lijalo.

Walinzi wa taifa zaidi ya elfu moja tayari wameandaliwa kwa ajili ya zoezi la ukozi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.