Pata taarifa kuu
MAREKANI-HOUSTON- HALI YA HEWA

Kimbuga Harvey chasababisha mafuriko makubwa Houston

Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga cha Harvey yameuacha mji wa Houston ambao ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Marekani katika hali mbaya huku uwanja wake wa ndege na barabara kuu vikilazimika kufungwa huku mamia ya makazi ya raia yakijaa maji.

Ndege iliyoharibiwa nakimbunga Harvey kwenye uwanja wa ndege karibu na mji wa Fulton, Texas, Agosti 26, 2017.
Ndege iliyoharibiwa nakimbunga Harvey kwenye uwanja wa ndege karibu na mji wa Fulton, Texas, Agosti 26, 2017. REUTERS/Rick Wilking
Matangazo ya kibiashara

Viwanja viwili vya ndege kwenye mji huo vilifungwa huku hospitali muhimu nazo zikilazimika kuwahamisha wagonjwa, katika mafuriko ambayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu watatu.

Kitengo cha maafa nchini Marekani kimesema mafuriko haya hayajawahi kushuhudiwa katika historia za vimbunga vilivyoikumba nchi hiyo. Watu zaidi ya watu elf mbili wameokolewa.

Maelfu ya raia wameokolewa huku watalaamu wakionya kuwa mafuriko zaidi yanatarajiwa.

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika jimbo laTexas kufuatia Kimbunga Harvey, ambacho kimekua sasa dhoruba ya kitropiki.

Upepo wenye kasi ya kilomita 215 kwa saa ulipiga pwani kadhaa siku ya Jumamosi, wakazi wengi walikimbilia kwenye mahandani na mafuriko makubwa yaanatarajiwa siku zijazo. Athari za kiuchumi pia zinaweza kuwa kubwa.

Kwa tahadhari, robo ya vifaa vua mafuta katika Ghuba ya Mexico vimefungwa kabla ya kupita kwa kimbunga hiki. Kiwango cha uharibifu hakijaijulikana bado, lakini Mamlaka ya Dharura nchini Marekani imebaini kwamba itachukua miaka kadhaa kwa kufuta athari za janga hili.

Texas, ambayo imekumbwa na kimbunga Harveyi ni, baada ya California, jimbo la pili lenye nguvu zaidi nchini Marekani katika masuala ya kiuchumi. Jimbo hili lingelikua huru, uchumi wake ungekuwa katika kiwango cha kile cha Uhispania au Canada.

Texas huzalisha asilimia 20 ya mafuta ya ya Marekani na 30% ya gesi asilia. Pia ni jimbo la pili kwa kilimo, hasa kwa mifugo na pamba. Kiwango cha ukosefu wa ajira kiko chini ya wastani wa kitaifa.

Na, kwa miaka 30 Texas ilipanda kiuchumi. Imekuwa kitovu muhimu kwa maendeleo ya teknolojia mpya, umeme, programu ya bioteknolojia na ujenzi wa viwanja vya ndege. Texas inatoa 10% ya uzalishaji wa umeme na 10% ya uzalishaji wa saruji na matofali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.