Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Mgomo dhidi ya Katiba mpya ya Maduro waendelea Venezuela

Makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yalizuka siku ya Jumatano Julai 26 nchini Venezuela, na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wakati wa mgomo wa saa 48 uliyoandaliwa na upinzani dhidi ya uchaguzi wa Jumapili wa wabunge watakaosimamia katiba mpya.

Waandamanaji wakikabiliana na vikodsi vya usalama wakati wa mgomo wa jumla kuhusu uchaguzi wa Katiba uliopendekezwa na rais Maduro, Caracas Julai 26, 2017.
Waandamanaji wakikabiliana na vikodsi vya usalama wakati wa mgomo wa jumla kuhusu uchaguzi wa Katiba uliopendekezwa na rais Maduro, Caracas Julai 26, 2017. REUTERS/Marco Bello
Matangazo ya kibiashara

Mtu aliyeuawa wakati wa maandamano katika jimbo la Merida (magharibi mwa Venezuela), alikua na umri wa miaka 30. Mahakama imeanzisha uchunguzi. Idadi ya watu ambao wameuawa katika maandamano hayo yaliyoanza miezi minne iliyopita imefikia 103, huku maelfu ya watu wakijeruhiwa na maelfu wengine wakiendelea kushikiliwa.

Barabara na mita mbalimbali iko patupu, maduka yamefungwa, shughuli mbalimbali zimesimama katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Katika miji kama maeneo mbalimbali ya mji wa Caracas, hasa katika ngome za upinzani kama vile kusini mashariki mwa mji wa Caracas, lakini pia katika maeneo ya kibiashara kama vile Altamira au katikati mwa mji Chacao, shughuli zimekwama tangu siku ya Jumatano asubuhi.

Wananchi wa Venezuela wameamua kubakia nyumbani, kufuatia wito uliotolewa na upinzani. Mgomo huu wa saa 48 unafanyika baada ya ule wa saa 24 ambao ni wa kwanza kufanyika nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja, uliofanyika wiki jana.

Katika miji mingine kulishuhudiwa maandamano ambapo waandamanaji walikabiliana na polisi huku polisi ikilazimika kutumia nguvu zaidi kwa kuwatawanya.

Katika makabiliano ya wiki jana waandamanaji watatu waliuawa, wengine wengi kujeruhiwa na baadhi kukamatwa, kwa mujibu wa mashahidi.

Hatua hiyo ni kupinga mipango ya serikali ya kuandika tena katiba mpya, huku rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu.

Upinzani unadai kuwa rais Maduro anajaribu kujiimarisha madarakani kwa kubadili katiba, hali ambayo itabadili hali ya sasa ya upinzani kudhibiti bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.