Pata taarifa kuu
VENEZUELA-USALAMA

Upinzani wahamasishwa kwa maandamano Venezuela

Nchini Venezuela, upinzani umetoa wito kwa mgomo wa jumla wa saa 48 kuanzia siku ya JumatanoJulai 26. Lengo lake ni kumshinikiza rais Nicolas Maduro kuondoa bungeni rasimu yake ya marekebisho ya katiba.

Upinzani waafanya mgomo wa siku mbili kuanzia Jumatano Julai 26 hadi Alhamisi dhidi Rais Maduro.
Upinzani waafanya mgomo wa siku mbili kuanzia Jumatano Julai 26 hadi Alhamisi dhidi Rais Maduro. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi nchini Venezuela umepangwa kufanyika Julai 30, huku upinzani ukidai kuwa hoja ya marekebisho ya katiba ni "wizi kwenye Katiba".

Imekuwa karibu miezi minne upinzani ukuindamana dhidi ya serikali Kichavez na tangu maandamano kuanza, zaidi ya watu 100 wameuawa. Wiki hii ni muhimu na yenye maamuzi kabla ya kura ya maoni kuhusu Katiba iliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili Jula 30. Wakati unakwenda kwa upande wa upinzani, na mgomo uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano na Alhamisi ni moja ya hatua ya muhimu zilizotolewa na upinzani.

Siku ya Jumanne usiku, Makamu wa Spika wa Bunge aliwatolewa wito wananchi waVenezuela "kufanya kilio chini ya uwezo wao". Changamoto ni kufanya kinachowezekana kuongeza shinikizo kwa Rais Maduro ikiwa zimesalia siku nne tu kabla ya uchaguzi kuhusu mageuzi ya katiba yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumapili.

Upinzani ulionya, ukitangaza "wiki ambayo itatalazimika kutumia nguvu ya kiroho na nguvu ya kila mmoja." Baada ya mgomo wa siku ya Alhamisi iliyopita, upinzani umeendelea kusisitiza wakati huu ukiwataka wafuasi wake kufanya mgomo wa siku mbili kuanzia siku ya Jumatano Julai 26 saa 06:00 asubuhi saa za Venezuela.

Wakazi katika mji mbalimbali walitumia siku ya jana kununua chakula kwa wingi kwa kujiandaa na mgomo huo, licha ya uhaba wa chakula unaoshuhudiwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.