Pata taarifa kuu

Nigeria: watu kadhaa wafariki wakati wa mkanyagano kaskazini mwa nchi

Takriban wanawake wanne walifariki siku ya Jumapili wakati wa mkanyagano katika mji wa Bauchi, kaskazini mwa Nigeria, kulingana na polisi. Lakini kulingana na vyanzo vingine vya ndani, idadi hii inaweza kuwa mara nne zaidi. Watu kumi na saba - watoto kumi na wanawake saba waliofariki - waliripotiwa kuhamishwa hospitalini kati ya wengi waliojeruhiwa.

Polisi ya Nigeria huko Bauchi, kaskazini mwa Nigeria
Polisi ya Nigeria huko Bauchi, kaskazini mwa Nigeria AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili umati mkubwa wa watu hasa wanawake na watoto ulikusanyika mbele ya ofisi za kampuni ya Shafa Holding inayojishughulisha na masuala ya mafuta.

Kila mtu alitarajia kupokea mchango wa naira 5,000 (karibu euro 3.10). Ugawaji huu wa pesa uliandaliwa na mmiliki wa kampuni hiyo kwa ajili ya kunusuru familia na kuzisaidia kununua chakula katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Lakini walengwa, wengi zaidi kuliko ilivyotarajiwa, walikimbilia kupokea msaada huu. Baada ya mkasa huu, wanawake wasiopungua watano walipokelewa wakiwa katika hali mbaya katika hospitali hiyo katika mji wa Bauchi, ulioko katika eneo la Kaino.

Hii ni mara ya pili wiki hii kwa Nigeria kukumbwa na aina hii ya ajali. Siku ya Ijumaa, wanafunzi wawili walipoteza maisha wakati wa usambazaji wa chakula kwenye chuo kimoja, zoezi lililoandaliwa katikati mwa nchi, katika jimbo la Nasarawa.

Kwa sasa Nigeria inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na inajitahidi kumaliza umaskini. Bei za vyakula zimeongezeka mara tatu katika wiki za hivi karibuni. Mfumuko wa bei ulifikia 31.7% mwezi Februari, kiwango cha juu zaidi kilichorekodiwa nchini Nigeria katika miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.