Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Nigeria: Zaidi ya watu 100 watekwa nyara

Zaidi ya watu 100 wametekwa nyara kaskazini-magharibi mwa Nigeria katika mashambulizi mawili tofauti, huku wimbi jipya la utekaji nyara likisumbua mamlaka ya Rais Bola Ahmed Tinubu, ambaye aliapa kukabiliana na ukosefu wa usalama.

Kajuru, katika Jimbo la Kaduna, ambapo watu wenye silaha waliwateka nyara watu 87 usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, , kulingana na kiongozi wa serikali ya mtaa, Ibrahim Gajere.
Kajuru, katika Jimbo la Kaduna, ambapo watu wenye silaha waliwateka nyara watu 87 usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, , kulingana na kiongozi wa serikali ya mtaa, Ibrahim Gajere. © Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Utekaji nyara huu mwingine katika Jimbo la Kaduna unafuatia ule wa watu dazeni kadhaa wiki iliyopita katika wilaya moja ya Kajuru, na vile vile mwanzoni mwa mwezi Machi wa zaidi ya wanafunzi 250 kutoka shule ya Kuriga, kilomita 150 kutoka Kajuru. Utekaji nyara huu mpya wa watu wengi katika nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika ulifanyika mwishoni mwa juma.

Wakati wa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, watu wenye silaha waliwateka nyara watu 87 katika eneo la Kajuru Station, kulingana na kiongozi wa serikali ya mtaa, Ibrahim Gajere. "Walienda kuchukua watu kutoka majumbani mwao wakiwa wamewaelekezea bunduki," ameliambia shirika la habari la AFP.

Harisu Dari, ambaye nimkazi wa eneo hilo, amesema makundi ya washambuliaji, wanaojulikana kama majambazi, walivamia kijiji hicho mwendo wa saa nne usiku na kwenda nyumba kwa nyumba kuwateka nyara wakaazi.

Chanzo cha Umoja wa Mataifa na afisa wa zamani wa eneo hilo, wote wakizungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina, wamethibitisha tukio hilo. Siku ya Jumamosi, watu 16 walitekwa nyara huko Dogon Noma, yapata kilomita kumi kutoka eneo hilo , kulingana na Harisu Dari, chanzo cha Umoja wa Mataifa na afisa wa zamani wa eneo hilo.

Wiki iliyopita, watu wenye silaha waliwateka nyara makumi ya watu katika kijiji kingine wilayani Kajuru.

"Vitendo kama vya utekaji nyara hujirudia"

Magenge ya wahalifu mara nyingi huteka nyara watu wengi kaskazini-magharibi mwa Nigeria, yakilenga shule, vijiji na barabara kuu ambapo wanaweza kuteka nyara haraka idadi kubwa ya watu ili wapate fidia. Mapema mwezi huu, zaidi ya wanawake na watoto 100 walitekwa nyara kutoka kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo la Borno (kaskazini magharibi) na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi.

Kisha watu wenye silaha waliwateka nyara zaidi ya wanafunzi 250 kutoka shule moja katika kijiji cha Kuriga, takriban kilomita 150, katika mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kutokea kwa miaka mingi. Siku chache baadaye, wanafunzi wasiopungua 15 kutoka shule ya Kiislamu katika jimbo la Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria walitekwa nyara na watu wenye silaha, kulingana na vyanzo vya ndani.

Mawimbi haya yanayofuatana ya utekaji nyara ya watu wengi yanajumuisha changamoto kubwa kwa mkuu wa nchi. Wiki iliyopita, alisema aliviagiza vyombo vya usalama kutolipa fidia ili wanafunzi hao waachiliwe. Wazazi wa watoto hao wanasema watekaji nyara walidai malipo makubwa ili watoto hao waweze kuachiliwa.

Nchini Nigeria, waathiriwa wa utekaji nyara mara nyingi huachiliwa kufuatia mazungumzo na mamlaka, ingawa maafisa wanakanusha kuwa fidia hulipwa. Familia na jumuiya nzima hukusanya akiba zao ili kulipa fidia, lakini sheria ya mwaka 2022 inakataza kupeana pesa kwa watekaji nyara. Familia nyingi zinasema kuwa haziamini mamlaka na hazina chaguo.

"Vijana wote ambao hawaoni mustakabali wa Nigeria, kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, wanajihusisha na utekaji nyara ili kupata fidia kama njia ya kujikimu," Confidence MacHarry, wa shirika la kutoa usauri wa usimamizi wa hatari la SBM Intelligence ameliamia shirika la habari la AFP .

"Tulichoona hadi sasa katika majibu ya serikali huwa ni kitu kimoja, kusita kati ya 'hatutalipa fidia' na 'tunafanya kila tuwezalo kuwarudisha watoto nyumbani kwao", kulingana na Confidence MacHarry. "Kwa hivyo, mwisho wa siku, kila wakati inarudi kwenye mazungumzo nyuma ya pazia, kulipa fidia, kupunguza usalama shuleni na, mara nyingi zaidi,hali kama hiyo hujirudia," ameongeza.

Shirika la SBM Intelligence limesema kuwa limerekodi watu 4,777 waliotekwa nyara tangu Bw Tinubu aingie madarakani mwezi Mei 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.