Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Nigeria: Zaidi ya wanafunzi 200 waliotekwa nyara mapema Machi waachiliwa

Wanafunzi zaidi ya 200 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule ya kaskazini-magharibi mwa Nigeria mapema mwezi Machi wameachiliwa, gavana wa jimbo la Kaduna ametangaza leo Jumapili. "Watoto wa shule ya Kuriga ambao walitekwa nyara wameachiliwa na salama salimini," Gavana Uba Sani amesema kwenye taarifa, bila kutaja jinsi walivyoachiliwa.

Muonekano wa shule ya Kuriga, ambapo mnamo Machi 8, zaidi ya wanafunzi 250 walitekwa nyara, katika eneo la Kaduna, Nigeria.
Muonekano wa shule ya Kuriga, ambapo mnamo Machi 8, zaidi ya wanafunzi 250 walitekwa nyara, katika eneo la Kaduna, Nigeria. © HAIDAR UMAR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliagiza vikosi vya usalama mnamo Machi 13 kutolipa fidia ya kuachiliwa kwao. Kulingana na familia za waathiriwa, watekaji nyara walikuwa wamedai malipo makubwa.

Sheria iliwekwa mwaka wa 2022 inapiga marufuku kuwapa wateka nyara pesa. Lakini katika miaka ya hivi majuzi, mamia ya watoto wa shule na wanafunzi wametekwa nyara, haswa katika Jimbo la Kaduna.

Utekaji nyara wa watu wengi, tatizo kubwa

Waathiriwa wa utekaji nyara kwa kawaida huachiliwa muda mfupi baadaye kufuatia mazungumzo na mamlaka za ndani, ingawa maafisa wa serikali bado wanakanusha kuwa fidia zililipwa. Kwa kawaida, familia na vijiji vizima hukusanya akiba zao ili kulipa fidia kwa sababu wanabaini hawana chaguo.

Utekaji nyara mkubwa na madai ya fidia ili kuwaachilia watu waliotekwa nyara ni tatizo kubwa na huathiri nchi nzima, yenye watu wengi zaidi katika bara la Afrika. Hapo zamani, magenge ya wahalifu waliojihami vikali kwa silaha yalilenga shule, haswa kaskazini magharibi mwa nchi.

Mnamo Februari 2021, watu wenye silaha walishambulia shule ya wasichana katika mji wa Jangebe, katika jimbo la kaskazini la Zamfara, na kuwateka nyara zaidi ya watu 300. Mapema mwezi Machi, zaidi ya wanawake 100 walitoweka kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya utekaji nyara mkubwa uliohusishwa na wanajihadi.

Katika miaka ya hivi karibuni, magenge ya wahalifu yameshambulia shule, hasa katika maeneo ya mashambani ya majimbo ya kaskazini magharibi mwa Nigeria. Rais Bola Ahmed Tinubu, aliyeingia madarakani mwaka 2023, aliahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama, unaochochewa na makundi ya wanajihadi, majambazi kaskazini mashariki na kuzuka kwa ghasia kati ya jamii katika majimbo ya kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.