Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu amelitaka jeshi kuwakamata wahusika wa mauaji ya wanajeshi 16

Nairobi – Rais wa Nigeria Bola Tinubu amelitaka jeshi la nchi yake kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya wanajeshi 16 waliouawa wakiwa kwenye harakati za kuhakikisha amani kusini mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, maofisa wake walikuwa wakijibu makabiliano kati ya jamii ya Okuama na Okoloba katika jimbo lenye utajiri wa mafuta kusini mwa Delta, waliposhambuliwa na kundi la vijana.

Rais Tinubu alisema kuwa raia aliuawa katika kile alichokiita kama "shambulio la moja kwa moja kwa taifa letu".

Jeshi la Nigeria lilisema Jumamosi kwamba uchunguzi unaendelea na watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya kamanda wa jeshi, maofisa wawili wenye cheo cha Meja na kapteni  mmoja pamoja na wanajeshi 12 wakati wa shambulio hilo.

Mapema Jumapili, ripoti zilisema kuwa baadhi ya maeneo kwenye jamii husika zilichomwa moto na vikundi visivyojulikana huku wanakijiji wakikimbia eneo hilo kwa hofu ya mashambulio ya kulipiza kisasi kutoka kwa jeshi la nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Tukur Gusau  alisisitiza kuwa jeshi lazima lipate silaha zilizochukuliwa kutoka kwa maofisa waliouawa.

Jamii hasimu zimekuwa zikikabiliana mara kwa mara kuhusu umiliki wa ardhi na haki za uvuvi katika majuma ya  hivi karibuni, na kuacha watu kadhaa wakiwa wameuawa, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.