Pata taarifa kuu

Nigeria: Wanajeshi 16 wameuawa wiki hii katika jimbo la Delta

Nairobi – Nchini Nigeria, wanajeshi 16 wameuawa wiki hii katika jimbo la Delta, wakati walipokuwa wamekwenda kutuliza mapigano kati ya wanakijiji ambao wamekuwa wakipigana.

Uongozi wa kijeshi umethibitisha mauaji ya maafisa wake, waliowazingira na kuwauwa baada ya kuja kutuliza mzozo wa ardhi
Uongozi wa kijeshi umethibitisha mauaji ya maafisa wake, waliowazingira na kuwauwa baada ya kuja kutuliza mzozo wa ardhi AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa kijeshi umethibitisha mauaji ya maafisa wake, waliowazingira na kuwauwa baada ya kuja kutuliza mzozo wa ardhi katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta.

Brigedia Jenerali Tukur Gusau amesema wanajeshi hao waliokua wamekwenda kwenye kijiji cha Okuoma kusaidia kuleta utulivu, walishambuliwa na vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha.

Kufuatia tukio hilo, Wizari ya ulinzi, imeagiza kuchunguzwa kwa tukio hilo na wale wote waliohusika, wachukuliwe hatua.

Aidha, amethibitisha kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na kinachoendelea ni uchunguzi wa ni kwanini walitekeleza mauaji hayo.

Mapigano ya wakaazi katika jimbo la Delta, hutokea mara kwa mara kuhusu ardhi na kushinikiza malipo kutoka kwa kampuni za kuchimba mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.