Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Nigeria: Zaidi ya wanawake 100 hawajulikani walipo baada ya utekaji nyara wa watu wengi

Zaidi ya wanawake 100 wametoweka kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya utekaji nyara mkubwa unaohusishwa na wanajihadi, vyanzo rasmi vimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi, na kuongeza makadirio ya hapo awali ambayo yaliripoti kuwa takriban wanawake 47 walitekwa nyara. 

Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria, Oktoba 2019. (Picha ya kielelezo).
Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria, Oktoba 2019. (Picha ya kielelezo). AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea wiki iliyopita katika kijiji cha Ngala, nchini Nigeria, lakini taarifa nyingi bado hazijaweka wazi mazingira ya watu hao kutoweka,  ikiwa ni pamoja na idadi kamili ya watu waliotoweka. 

Viongozi wa wanamgambo wanaopinga wajihadi wanalishutumu kundi la islamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP) kwa kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Borno, linalokabiliwa na uasi wa wanajihadi ambao wameua zaidi ya watu 40,000 watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao tangu mwaka 2009. Ali Bukar, afisa wa kitengo cha habari cha serikali ya mtaa wa Ngala, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wakazi wa Ngala wamethibitisha kutoweka kwa watu 113.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), shambulio hilo lilitekelezwa Februari 29 na zaidi ya watu 200 waliokuwa wakiishi katika kambi za wakimbizi walitekwa nyara walipokuwa wakiokota kuni. OCHA imeliambia shirika la habari la AFP kuwa takwimu hii ilitokana na makadirio ya viongozi wa mitaa, na kufafanua kuwa ukaguzi bado unaendelea katika kambi nne za wakimbiziwa ndani.

Utekaji nyara, changamoto kuu nchini Nigeria

Mnamo Jumanne Machi 5, kiongozi wa wanamgambo wanaopinga jihadi, Shehu Mada, alibaini kuwa wanawake wanaotoka kwenye kambi za watu waliohamishwa walishambuliwa "na waasi wa ISWAP" Ijumaa iliyopita. "Baadhi ya wanawake waliweza kutoroka," Bw. Mada alieleza, akionyesha kwamba "wanawake 47" hawakuweza kupatikana.

Usman Hamza, kiongozi mwingine wa wanamgambo wanaopinga jihadi, alithibitishia AFP idadi hiyo siku ya Jumanne. Polisi bado hawajatoa takwimu kamili kuhusu idadi ya watu waliotekwa nyara.

Utekaji nyara nchini Nigeria, mara nyingi kwa ajili ya fidia, ni tatizo kubwa na huathiri nchi nzima. Mapema mwezi wa Februari, wanawake wasiopungua 35 waliokuwa wakirejea kutoka kwenye harusi walitekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini-magharibi la Katsina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.