Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wanawake 47 wa Nigeria washikiliwa mateka na wanajihadi

Takriban wanawake 47 hawajulikani waliko kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya utekaji nyara mkubwa uliofanywa na wanamgambo wa kijihadi, viongozi wa wanamgambo wanaopinga jihadi wameliambia shirika la Habari la AFP siku ya Jumanne.

Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara wa Chibok wakiwa na picha za binti zao wakati wa kumbukumbu mwaka wa 2019, miaka mitano baada ya kutekwa nyara na Boko Haram.
Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara wa Chibok wakiwa na picha za binti zao wakati wa kumbukumbu mwaka wa 2019, miaka mitano baada ya kutekwa nyara na Boko Haram. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa katika jimbo la Borno, linalokabiliwa na uasi wa wanajihadi ambao wamesababisha vifo vya watu zaidi ya 40,000 na milioni mbili kuyatoroka makazi yao tangu mwaka 2009, na lilitekelezwa na wanamgambo wa Islamic State huko Afrika Magharibi (ISWAP).

Wanawake katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Ngala, karibu na mpaka na Cameroon, walikuwa wakiokota kuni wakati "walipozingirwa na waasi wa ISWAP", mkuu wa wanamgambo wanapinga jihadi ameliiambia shirika la habari la AFP. "Baadhi ya wanawake waliweza kutoroka," ameongeza, lakini "wanawake 47 (...) hawakuweza kupatikana. Walitekwa nyara na wanajihadi," amesema.

Usman Hamza, kiongozi mwingine wa wanamgambo wanaopinga jihadi, amethibitisha takwimu hizi, akibaini kwamba "wanawake 47 (...) hawakurudi" knyumbani baada ya shambulio hilo. Kulingana na msemaji wa polisi wa jimbo la Borno Nahum Daso Kenneth, shambulio hilo lilitokea saa 10:00 alaasiri kwa saa za huko siku ya Ijumaa. Hata hivyo, polisi, haikutoa takwimu sahihi kuhusu idadi ya watu waliotekwa nyara.

Mwanachama wa huduma ya habari ya serikali ya mtaa wa Ngala, Ali Bukar, amesema amepokea ripoti za idadi kubwa zaidi ya wanawake waliotekwa nyara. Utekaji nyara nchini Nigeria, mara nyingi kwa ajili ya fidia, ni tatizo kubwa na huathiri nchi nzima. Magenge yanaendesha shughuli zao kwenye barabara kuu, katika nyumba za waathiriwa na hata shuleni; wanatekeleza kitendo hiki kutoka kwa kambi zinazopatikana katika misitu ya majimbo ya kaskazini-magharibi na kati ya nchi.

Mapema mwezi Februari, wanawake wasiopungua thelathini na watano waliokuwa wakirudi kutoka kwenye harusi walitekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la Katsina (kaskazini-magharibi). Rais Bola Ahmed Tinubu aliingia madarakani mwaka 2023 akiahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama, unaochochewa na makundi ya wanajihadi, majambazi kaskazini mashariki na kuongezeka kwa ghasia za kikabila katika majimbo ya kati. Lakini wakosoaji wanasema ghasia hizo hazijadhibitiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.