Pata taarifa kuu

Nigeria: Wanafunzi 17 wameambukizwa homa ya uti wa mgongo

Nairobi – Mamlaka nchini Nigeria imethibitisha kuwa karibia wanafunzi 17 kutoka shule tofauti katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo wamefariki baada ya kuambukizwa homa ya uti wa mgongo (Meningitis).

Idadi ya visa 473 vya maambukizo ya maradhi hayo vimethibitishwa na mamlaka kufikia sasa
Idadi ya visa 473 vya maambukizo ya maradhi hayo vimethibitishwa na mamlaka kufikia sasa Flickr/ Creative Commons
Matangazo ya kibiashara

Mohammed Sani-Idris, kamishena wa elimu kwenye jimbo hilo ameiambia BBC kuwa miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni kutoka shule za msingi na wengine kutoka shule za upili za bweni.

Visa 473 vya maambukizo ya maradhi hayo vimethibitishwa na mamlaka kufikia sasa.

Homa ya uti wa mgongo ni maambukizo ambayo husababisha kuvimba kwa baadhi ya sehemu za nje kwenye ubongo na uti wa mgongo.

Ugonjwa huo pia unaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu usipotambuliwa na  kutibiwa mapema.

Kwa mujibu wa wahudumu wa afya, ugonjwa huo unazuiwa tu kwa kuchomwa chanjo.

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Nigeria (NCDC) mapema mwezi huu kilikuwa kimetoa onyo kuhusu uwezekano wa kutokea kwa maradhi hayo.

Visa vingi vya maambukizo ya ugonjwa huo vimeripotiwa katika majimbo 19 kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.