Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Kanisa Katoliki na Protestanti wapaza sauti kuhusiana na auteuzi wa mwenyekiti wa CENI

Nchini DRC, mchakato wa kumteua mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi  (CENI) umesimamishwa. Katika mkutano na waandishi wa habari, Alhamisi, Oktoba 7, wawakilishi wa kanisa Katoliki na Protestanti walilaani jukumu la wanasiasa katika kuzuia mchakato huo.

Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO), huko Kinshasa, Desemba 21, 2016.
Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO), huko Kinshasa, Desemba 21, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine walifutilia mbali kuwania kwa Denis Kadima kwenye nafasi hiyo, ambaye wanamuona kuwa ana uhusiano wa karibu na rais Felix Tshisekedi na kusisitiza azma yao ya kupigania kuhakikisha, uchaguzi wa kuaminika unafanyika mwaka 2023.

Wawakilishi wa kanisa Katoliki na Protestanti wamekumbusha majaribio ya ufisadi kwa kutaka Denis Kadima aweze kuteuliwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CENI na vitisho vilivyotolewa na madhehebu mengine sita ya kidini. Na wanasema wana ushahidi usiopingika.

"Tumefanya mipango ya kurekodi mambo ambayo yatatuwezesha kujitetea ikiwa watabadilisha kauli kama walivyozoea," Padri Donatien N'shole, katibu mkuu wa Baraza kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO ), amesema . Viongozi wa kidini wanasema wako tayari kupeana ushahidi huu na ofisi ya Bunge.

Hakuna kurudi nyuma

Hawatarudi nyuma, ameonya Mchungaji Éric Nsenga, msemaji wa Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC): "Hata kama mkiwa watu milioni. Kamwe humuwezi kupata nafasi ikiwa mnasema uwongo. Ukweli unabaki kuwa ukweli. Tutaitetea hata kama tutabaki peke yetu. Tunamluamini Mungu kwa mimamo wetu ".

Wanataka uchaguzi wa wazi, ameongeza Padri Donatien N’shole, ambaye anasema ana hofu uwa mchakato huo utakumbwa na kasoro nyingi: "Wanataka kutupeleka katika mantiki ya mgombea mmoja". CENCO na ECC wanaahidi kutumia njia zote za kisheria, za kiraia, za kidemokrasia na za kichungaji kufanikisha uchaguzi wa wazi mnamo mwaka 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.