Pata taarifa kuu
DRC

Uchunguzi : DRC yashindwa kukabiliana vilivyo na Corona

Uchunguzi kutoka Chuo Kikuu kimoja jijini New York nchini Marekani, umebaini kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeshindwa kupambana ipasavypo na janga la Covid-19 kama ilivyoshuhudiwa wakati wa milipuko mingine ya magonjwa nchini humo.

Janga la Coronavirus nchini DRC: lazima uwe na pasi ili kuweza kutembea katika maeneo yaliyowekwa chini ya vizuizi vya watu kutotembea, Gombe, Kinshasa, Aprili 6, 2020.
Janga la Coronavirus nchini DRC: lazima uwe na pasi ili kuweza kutembea katika maeneo yaliyowekwa chini ya vizuizi vya watu kutotembea, Gombe, Kinshasa, Aprili 6, 2020. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, Shirika hilo la utafiti limebaini kuwa wakati kesi ya kwanza ya Covid-19 iliporipotiwa nchini DRC mwezi Machi mwaka 2020, nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na magojwa ya surua, kipindupindu na Ebola.

Imebainika kuwa mfumo wa afya nchini DRC hauna uwezo wa kudhibiti milipuko ya magonjwa nchini humo, na serikali nchini humo haipati msaada wa kutosha kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Licha ya serikali ya rais Felix Tshisekedi kuunda Kamati maalum ya kupambana na virusi vya Covid-19, kuna usimamizi na matumizi mabaya ya fedha zinazotengwa kuwasaidia wananchi kupambana na janga hilo.

Aidha, imeelezwa kuwa usambazwaji wa taarifa hauwafikii wahusika, lakini pia upinzani kati ya makundi mbalimbali yanachangia wagonjwa kutopewa huduma nzuri, lakini pia wahudumu wa afya wamekatishwa tamaa.

Ripoti hiyo imebaini kuwa, kati ya Dola Milioni 363 zilizotolewa na Shirika la Fedha duniani IMF kupambana na virusi vya Corona nchini humo, serikali imechapisha majarida 40 kwenye Tovuti ya Wizara ya afya kueleza kuwa imetumia tu Dola Milioni Sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.