Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

UN yatiwa wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu DRC

Miezi mitatu kabla ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, kuongezewa muda, Umoja wa Mataifa unasema unatiwa wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini humo. Mcongo mmoja kati ya watatu anategemea msaada, lakini msaada huo hauwezi kutolewa ipasavyo kwa sababu ya hali ya usalama.

Wakimbizi wa ndani katika kambi ya Bunia, Ituri, Aprili 12, 2018.
Wakimbizi wa ndani katika kambi ya Bunia, Ituri, Aprili 12, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Suala la uhaba wa chakula unaowakumba raia wa DRC lilikuwa katika ajenda ya mazungumzo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wanachama kumi na tano walikutana ili kutathmini hali nchini DRC na mahitaji kwa kikosi cha walinda amani.

Ukosefu wa usalama wa chakula

Lakini kwanza, Bintou Keita, mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anasema ana wasiwasi kuhusu hali halisi ya kibinadamu: 29% ya raia wa DRC wanakabiliwa na ukosefu wa chakula. Hali ni ngumu zaidi mashariki ya nchi, hasa katika mkoa wa Ituri. Mashambulizi dhidi ya shule na hospitali, idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani ilisababisha kuongezeka kwa mahitaji lakini hatari za usalama zinaendelea kutatiza zoezi la usambazaji wa misaada.

Kuongeza michango

Bintou Keita ametoa wito kwa nchi wanachama kuongeza michango yao kwa mpango wa majibu ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.