Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Marshal Khalifa Haftar apoteza imani kwa washirika wake

Wengi wanajiuliza iwapo mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya Marshal Khalifa Haftari bado ana nguvu za kuendeleza vita na serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli, baada ya vikosi vyake hivi karibuni kutimuliwa kwenye ngome zao.

Khalifa Haftar huko Benghazi, Oktoba 14, 2017.
Khalifa Haftar huko Benghazi, Oktoba 14, 2017. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Nchi za Misri na Urusi, ambazo ni washirika wa Marshal Khalifa Haftar, zimemteuwa kiongozi mwingine, Aguila Saleh, Spika wa Bunge, ili kuwakilisha eneo la Mashariki mwa Libya.

Nchi hizi zinalaumu kuona vikosi vya Marshal Khalifa Haftar hivi karibuni vilishindwa katika uwanja wa vita na kuendelea kupoteza baadhi ya maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao. Nchi nyingi za magharibi haziungi mkono uamuzi wa Marshal Haftar wa kukataa mkataba wa amani na kuendelea kukiuka makubaliano ambayo tayari yalikuwa yamefikiwa nchini Libya.

"Kuteua mtu mwingine kwenye nafasi ya Khalifa Haftar huko Magharibi mwa Libya itakuwa muhimu zaidi na, ni jambo la lazima" afisa mmoja wa Libya katika nchi ya kigeni amebaini.

Vyanzo vilivyo karibu na Bunge huko Benghazi vinasema kwamba Urusi, Marekani na Umoja wa Mataifa"wanatafuta kikamilifu kiongozi mwingine ambaye ataheshimu makubaliano kwa kipindi kijacho" hayo ni wakatio kambi ya Fayez al-Sarraj imekataa katu katu kuketi kwenye meza moja ya mazungumzo na Marshal Khalifa Haftar.

Hata hivyo Marshal Khalifa Haftar ametishia kumfunga Aguila Saleh, lakini kabila la Aguila Saleh, lenye watu wengi huko Mashariki mwa Libya limemuonya Khalifa Haftar kwa jaribio lolote la kumfunga Aguila Saleh.

Marshal Khalifa Haftar anashtumiwa kuangamiza maafisa wa jeshi lake ambao wamekuwa wakipinga hoja zake.

Jumanne 9 Juni, Mawaziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Italia na Ujerumani pamoja na afisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya, katika taarifa yao ya pamoja, walitoa wito wa kurejelea mazungumzo na kusitishwa kwa mapigano moto nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.