Pata taarifa kuu
LINYA-USALAMA-SIASA

Jeshi la serikali ya Tripoli laendelea na mashambulizi dhidi ya ngome za vikosi vya Haftar

Wanajeshi wa serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Wamesema wametekeleza shambulizi katika mji wa Sirte unaoshikiliwa na vikosi vya upinzani vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.

Libya inaendelea kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Libya inaendelea kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. ©REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Aidha, jeshi hilo limesema kuwa litaendelea na harakati za kuchukua ngome zaidi  zinazoshikiliwa na vikosi vya upinzani.

Yote haya yanakuja baada ya Misri kutangaza mpango wa usitishwaji wa vita kati ya pande zinazikinzana ili kuleta amani katika nchi hiyo ambayo imeshuhudia vita tangu mwaka 2011.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi Jumamosi alitangaza mpango wa kumaliza vita, akisema unajumuisha usitishwaji wa mapigano kuanzia leo Jumatatu, kwa lengo la kusafisha njia ya kufanyika uchaguzi "mpango huu pia unahakikisha uwakilishi wa haki wa maeneo yote matatu ya Libya katika baraza la rais, litakalochaguliwa na watu wa Libya chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ili wote waiongoze Libya kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo."

Wakati huo huo zaidi ya watu elfu 16 wamekimbia  makwao nchini humo, katika mapigano ya kukomboa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo lililokuwa linatawaliwa na wapiganaji wanaongozwa na Khalifa Haftar, umesema umoja wa mataifa. 

Katika wiki chache zilizopita wapiganaji wa serikali ya kitaifa ya umoja ya Tripoli (GNA) inayoungwa mkono na umoja wa mataifa  na Uturuki ,wamezidisha mashambulizi dhidi ya majeshi ya Haftar,  na kutwaa  ngome muhimu magharibu mwa nchi ukiwemo mji wa Tarhuna.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa umesema umetiwa moyo na miito ya kurejeshwa mazungumzo ya kumaliza mzozo nchini Libya, siku moja baada ya Misri kutangaza mpango wa amani wa upande mmoja ukiungwa mkono na serikali ya upande wa Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.