Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yaendelea kurindima Sirte, Libya

Mapigano yameendelea Jumatatu wiki hii huko Sirte, nchini Libya licha ya wito wa kusitishwa mapigano kutoka Misri mwishoni mwa wiki hii iliyopita.

Vikosi vya Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya huko Tripoli Juni 4.
Vikosi vya Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya huko Tripoli Juni 4. REUTERS/Ayman Al-Sahili
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ushindi katika maeneo mbalimbali nchini humo bila hata hivyo kuwepo na mapigano yoyote, wiki iliyopita, vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa sasa vinakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vikosi vya Khalifa Haftar.

Vikosi vya Tripoli, vilivyo chini ya uongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa (GNA), vimetekeleza mashambulizi ya makombora katika mji wa Sirte mapema Jumatatu asubuhi. Kulingana na vyanzo katika uwabja wa vita, raia wasiopungua saba wameuawa, ikiwa ni pamoja na watoto watatu.

Wakati huo huo nchi kadhaa zimeunga mkono mpango wa Misri nchini Libya

Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE umesema unaunga mkono mpango wa amani wa Misri, baada ya ushindi kadhaa wa vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli inayotambuliwa kimataifa dhidi ya vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar. Waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya kigeni wa UAE, Anwar Garfash amesema leo kuwa juhudi hizo zinaimarisha kasi ya mataifa ya Kiarabu na kimataifa wa kusitisha haraka mapigano, kuondolewa kwa majeshi ya kigeni na kurejea kwa mfumo wa kisiasa

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi Jumamosi alitangaza mpango wa kumaliza vita, akisema unajumuisha usitishwaji wa mapigano kuanzia leo Jumatatu, kwa lengo la kusafisha njia ya kufanyika uchaguzi "mpango huu pia unahakikisha uwakilishi wa haki wa maeneo yote matatu ya Libya katika baraza la rais, litakalochaguliwa na watu wa Libya chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ili wote waiongoze Libya kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo."

Zaidi ya watu elfu 16 wamekimbia makwao nchini humo, katika mapigano ya kukomboa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo lililokuwa linatawaliwa na wapiganaji wanaongozwa na Khalifa Haftar, umesema umoja wa mataifa.

Katika wiki chache zilizopita wapiganaji wa serikali ya kitaifa ya umoja ya Tripoli (GNA) inayoungwa mkono na umoja wa mataifa na Uturuki ,wamezidisha mashambulizi dhidi ya majeshi ya Haftar, na kutwaa ngome muhimu magharibu mwa nchi ukiwemo mji wa Tarhuna.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa umesema umetiwa moyo na miito ya kurejeshwa mazungumzo ya kumaliza mzozo nchini Libya, siku moja baada ya Misri kutangaza mpango wa amani wa upande mmoja ukiungwa mkono na serikali ya upande wa Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.