Pata taarifa kuu
LIBYA-ERDOGAN-USALAMA-SIASA

Erdogan: Tumeafikiana na Trump kuhusu mzozo wa Libya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema yeye na rais wa Marekani Donald wameafikiana kuhusu maswala kadhaa kuhusu mzozo wa Libya baada ya kufanya mazungumzo ya simu siku ya Jumatatu.

Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya angani kwenye uwanja wa ndege wa Mitiga huko Tripoli, Libya, Mei 10, 2020.
Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya angani kwenye uwanja wa ndege wa Mitiga huko Tripoli, Libya, Mei 10, 2020. REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Erdogan hata hivyo amesisitiza ipo haja ya kufanya mazungumzo na rais wa Urusi Vladmir Putin, ambaye nchi yake imenyooshewa kidole kwa kutuma mamluki kuwasaidia wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar.

Uturuki inaunga mkono serikali ya umoja inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, sawia na Marekani japo washirika wake Misri na Umoja wa nchi za Kiarabu zinaunga mkono wapiganaji wa Haftar.

Mapema wiki hii Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE ulisema unaunga mkono mpango wa amani wa Misri, baada ya ushindi kadhaa wa vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli inayotambuliwa kimataifa dhidi ya vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar. Waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya kigeni wa UAE, Anwar Garfash amesema leo kuwa juhudi hizo zinaimarisha kasi ya mataifa ya Kiarabu na kimataifa wa kusitisha haraka mapigano, kuondolewa kwa majeshi ya kigeni na kurejea kwa mfumo wa kisiasa

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi Jumamosi alitangaza mpango wa kumaliza vita kwa lengo la kusafisha njia ya kufanyika uchaguzi "mpango huu pia unahakikisha uwakilishi wa haki wa maeneo yote matatu ya Libya katika baraza la rais, litakalochaguliwa na watu wa Libya chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ili wote waiongoze Libya kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo."

Zaidi ya watu elfu 16 wamekimbia makwao nchini humo, katika mapigano ya kukomboa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo lililokuwa linatawaliwa na wapiganaji wanaongozwa na Khalifa Haftar, umesema Umoja wa Mataifa.

Katika wiki chache zilizopita wapiganaji wa serikali ya kitaifa ya umoja ya Tripoli (GNA) inayoungwa mkono na umoja wa mataifa na Uturuki ,wamezidisha mashambulizi dhidi ya majeshi ya Haftar, na kutwaa ngome muhimu magharibu mwa nchi ukiwemo mji wa Tarhuna.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa umesema umetiwa moyo na miito ya kurejeshwa mazungumzo ya kumaliza mzozo nchini Libya, siku moja baada ya Misri kutangaza mpango wa amani wa upande mmoja ukiungwa mkono na serikali ya upande wa Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.