Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Vikosi vya serikali ya Tripoli vyatangaza kudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa

Vikosi tiifu kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli (GNA) vimetangaza kuwa "vimeudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli" kutoka mikononi mwa majeshi ya Marshal Khalifa Haftar.

Vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) kwenye uwanja wa ndege wa imataifa wa Tripoli, Juni 3, 2020.
Vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) kwenye uwanja wa ndege wa imataifa wa Tripoli, Juni 3, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo linaofuata mapigano makali ambayo yalitokea, kwa siku kadhaa karibu na uwanja huo wa ndege.

Shambulio dhidi ya uwanja wa ndege lilizinduliwa Jumatano asubuhi na vikosi vikosi vya serikali ya Tripoli, vikisaidiwa na ndege zisizokuwa na rubani za Uturuki na mamluki kutoka Syria.

Baada ya majeshi ya serikali kudhibiti uwanja wa ndege wa kitamatifa wa Tripoli, vikosi vya Khalifa Haftar viliondoka na kuelekea Kusini mwa mji huo.

Tangu Mei 26, vikosi tiifu kwa serikali ya umoja wa kitaifa vimekuwa vikipata ushindi katika uwanja wa vita. Kudhibitiwa kwa uwanja wa ndege wa Tripoli, ni ushindi mkubwa kwa majeshi haya, kwani uwanja huo wa ndege, ni eneo la kimkakati.

Hivi karibuni vikosi vya Marshal Khalifa Haftar (LNA) na serikali ya umoja wa kitaifa ilio madarakani huko Tripoli walikubaliana kuanza tena mazungumzo kwa lengo la kusitisha mapigano, baada ya wiki kadhaa za mapigano nje ya mji mkuu Tripoli.

Mikataba ya kusitisha mapigano imefikiwa mara kadhaa mwaka huu, lakini bado haijatekelezwa. Ghassan Salame, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, alijiuzulu mwezi Machi mwaka huu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado halijamteua mrithi wake, hali ambayo imeendelea kutatiza juhudi za amani.

Nchi za kigeni kuingilia kijeshi nchini Libya ni hali ambayo imeendelea kuongeza machafuko. Wiki iliyopita Marekani ilitangaza kwamba ndege 14 za kijeshi kutoka Urusi zilipelekwa katika kambi ya kikosi cha wanamaji cha majeshi ya Marshal Khalifa Haftar katikati mwa Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.