Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI-URUSI-USALAMA

Jeshi la Marekani lashutumu Urusi kwa kupeleka ndege za kivita nchini Libya

Marekani inasema Urusi, ilituma ndege zake za kivita kuwasaidia mamluki wake wanaomsaidia kiongozi wa upinzani nchini Libya, Jenerali Khalifa Haftar.

"Urusi inajaribu kuchochea vita nchini Libya kwa maslahi yake binafsi," mkuu wa majeshi ya Marekani barani Afrika, Stephen J. Townsend amesema katika taarifa kutoka makao yake makuu huko Stuttgart, Ujerumani.
"Urusi inajaribu kuchochea vita nchini Libya kwa maslahi yake binafsi," mkuu wa majeshi ya Marekani barani Afrika, Stephen J. Townsend amesema katika taarifa kutoka makao yake makuu huko Stuttgart, Ujerumani. www.africom.mil
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya jeshi la Marekani linalofanya operesheni zake barani Afrika siku ya Jumanne ilisema: Moscow hivi majuzi ilipeleka ndege za kijeshi nchini Libya ili kulisaidia jeshi la Urusi la kibinafsi linaloungwa mkono na serikali ya Urusi linalotekeleza operesheni zake ardhini, lilisema.

Ripoti zinasema kuwa, ndege hizo za kivita zilisimama nchini Syria, kabla ya kwenda nchini Libya lakini haijafamika ni lini ndege hizo zilifika nchini humo.

Kulingana na gazeti la al Sabah nchini humo ndege nane za Urusi aina ya MiG-29 na Su-24 zilisafiri kutoka Syria kuelekea Libya ili kusaidia jeshi la jenerali haftar.

Wakati huo huo, serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inasema kuwa mamluki hao wameanza kuondoka katika kambi walizokuwa wamefikia.

Uturuki inaunga mkono jeshi linalotambulika na Umoja wa kimataifa la GNA mjini Tripoli.

Urusi haijathibitisha uwepo wa mamluki wa kundi la Wagner nchini Libya.

Kulingana na serikali ya muungano GNA inayotambulika na Umoja wa Mataifa, zaidi ya wapiganaji 1,000 wa kundi la Wagner walitoroka eneo moja Kusini mwa Tripoli wakiabiri ndege za kusafirishia mizigo za Urusi baada ya kusukumwa nyuma na wanajeshi wa GNA.

Hata hivyo serikali ya Urusi imekana kushirikishwa na kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.