Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-SIASA-USALAMA

UN: Kambi zinazohasimiana nchini Libya zakubali kuanzishwa mazungumzo

Vikosi vya Marshal Khalifa Haftar (LNA) na serikali ya umoja wa kitaifa ilio madarakani huko Tripoli wamekubaliana kuanza tena mazungumzo kwa lengo la kusitisha mapigano, Umoja wa Mataifa umetangaza baada ya wiki kadhaa za mapigano nje ya mji mkuu Tripoli.

Mikataba ya kusitisha mapigano nchini Libya imefikiwa mara kadhaa mwaka huu, lakini bado haijatekelezwa.
Mikataba ya kusitisha mapigano nchini Libya imefikiwa mara kadhaa mwaka huu, lakini bado haijatekelezwa. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni kwenye tovuti, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umekaribisha makubaliano ya pande hasimu nchini Libya kuanza tena mazungumzo kwa muundo wa "5 + 5", unaojumuisha maafisa wakuu watano kutoka pande zote mbili.

Vikosi vya ANL, vinavyodhibiti mashariki mwa nchi, vimekuwa vikijitahidi bila mafanikio kuuteka mji wa Tripoli tangu mwezi Aprili 2019. Vikosi vitiifu kwa serikali ya umoja ya kitaifa ya Libya, yenye makao yake mjini Tripoli, ambavyo vinasaidiwa na Uturuki, hivi karibuni viliyatimua majeshi ya Marshal Khalifa Haftar katika maeneo kadhaa karibu na mji mkuu Tripoli, lakini wmajeshi hayo, yanayosaidiwa na Falme za Kiarabu, Urusi na Misri, wamesema wanadhibiti maeneo hayo tangu Jumatatu wiki hii.

Mikataba ya kusitisha mapigano imefikiwa mara kadhaa mwaka huu, lakini bado haijatekelezwa. Ghassan Salame, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, alijiuzulu mwezi Machi mwaka huu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado halijamteua mrithi wake, hali ambayo imeendelea kutatiza juhudi za amani.

Nchi za kigeni kuingilia kijeshi nchini Libya ni hali ambayo imeendelea kuongeza machafuko. Wiki iliyopita Marekani ilitangaza kwamba ndege 14 za kijeshi kutoka Urusi zilipelekwa katika kambi ya kikosi cha wanamaji cha majeshi ya Marshal Khalifa Haftar katikati mwa Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.