Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Libya: Wahamiaji kadhaa wauawa na kundi wafanyabiashara haramu

Mtu mmoja aliyekuwa akijihusisha na biashara haramu ya binadamu aliuawa hivi karibuni katika kituo haramu cha wakimbizi katika mji wa Mizdah, kinachopatikana zaidi ya kilomita 150 Kusini magharibi mwa Tripoli, karibu na Zintane.

Wahamiaji wameonekana katika kituo cha wakimbizi ya Zawiyah, kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, Juni 17, 2017.
Wahamiaji wameonekana katika kituo cha wakimbizi ya Zawiyah, kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, Juni 17, 2017. Taha JAWASHI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Familia ya mfanyabiashara huyo na wafuasi wake wamejilipiza kisasi kwa kuwauwa zaidi ya wahamiaji 30, ambao wengi wao ni kutoka Bangladesh.

Tukio hilo lilitokea Jumatano Mei 27 karibu 5:00. Kulingana na mashahidi, kutokubaliana kati ya mfanyabiashara huyo na wahamiaji wakati walipofikishwa katika kituo hicho ndio sababu ya kifo chake. Mfanyabiashara huyo anayefahamika kwa shughuli zake hizo haramu alimuua mmoja wa wahamiaji hao kabla ya kuuawa na wahamiaji wengine.

Wakati huo huo ndugu wa mfanyabiashara huyo haramu walipowasili eneo la tukio walilipiza kisasi na kuua wahamiaji 26 kutoka Bangladesh na wanee kutoka nchi za Kiafrika, yaani wale wote ambao walikataa kuondoka katika kituo hicho haramu cha wahamiaji Wahamiaji wengine kumi na mmoja wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watano ambao wako katika hali mbaya, chanzo cha hospitali kimesema.

Kufuatia mauaji hayo, serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) imeahidi katika taarifa kuwa itawachukulia hatua kali wahalifu waliohusika na tukio hilo.

Maelfu ya wahamiaji wanasafiri kwenda Libya wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterranian kwenda Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.