Pata taarifa kuu
LIBYA-URUSI-USALAMA

Libya: Mamia ya mamluki kutoka Urusi waondolewa kwenye uwanja wa vita

Mamia ya mamluki wa Urusi Wanaoshirikiana na jenerali aliyeasi nchini Libya Khalifa Haftar wameondolewa katika mstari wa mbele wa mapambano na sasa wamepelekwa hadi Bani Walid, kilomita 170 Kusini Mashariki mwa Tripoli, vikosi vya serikali ya muungano wa kitaifa (GNA) vimesema.

Ghala la kambi ya jeshi la  wanaanga huko al-Watiya lililochukuliwa na jeshi la serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) kutoka mikononi mwa vikosi vya ANL vya Marshal Khalifa Haftar, Mei 18, 2020.
Ghala la kambi ya jeshi la wanaanga huko al-Watiya lililochukuliwa na jeshi la serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) kutoka mikononi mwa vikosi vya ANL vya Marshal Khalifa Haftar, Mei 18, 2020. REUTERS/Hazem Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wakuu wa vikosi vya serikali ya muungano wa kitaifa inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa wamefahamisha kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja vikosi vya Jenerali muasi Khalifa Haftar vilijaribu kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli bila mafanikio.

Taarifa ya vyombo vya usalama nchini Libya katika vikosi vya serikali ya muungano GNA, inasema ndege za kijeshi aina ya Antonov 32 iliwasafirisha mamluki wa kundi la Wagner la Urusi kati ya 1500 na 1600 kutoka eneo la mapambano hadi Bani Walid, mji ulioko umbali wa kilomita 170 Kusini Mashariki mwa Tripoli.

Tangu mwezi wa Januari mwaka huu Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamefahamisha kuwa mamluki hao wa kundi la Wagner Wamekuwa wakiunga mkono Jenerali muasi Khalifa Haftar nchini Libya tangu alipoanzisha uasi mwezi Aprili 2019, hakuna mazungumzo yoyote yaliyofikia kusainiwa kwa mkataba wa kusitishwa mapigano yaliyozaa matunda. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.