Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Mmoja wa wapinzani wakuu Sudan apinga mandamano ya nchi nzima

Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Sudan, Sadiq al-Mahdi amekataa wito wa kufanyika kwa maandamano ya nchi nzima kupinga wanajeshi kuongoza nchi hiyo.

Sadiq al-Mahdi, Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ummah, Khartoum Aprili 27, 2019.
Sadiq al-Mahdi, Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ummah, Khartoum Aprili 27, 2019. Auteur / Source / Crédit Ebrahim Hamid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matamshi yake yanakuja wakati huu kukiwa na mvutano kati ya baraza la kijesi na viongozi wa waandamanaji kuhusu muundo wa baraza la mpito litakaloshiriki kuandaa uchaguzi mpya.

Mapema wiki hii Serikali ya sasa ya kijeshi ya Khartoum ilifutilia mbali bila kupinga pendekezo la Ethiopia. Pendekezo ambalo lilikubaliwa siku ya Jumamosi na upinzani, na ambalo linataka kuwepo na baraza la mpito la watu kumi na tano, likiongozwa na idadi kubwa ya raia na na kuwepo na mfumo wa kupishana kwenye uongozi wa nchi kati ya jeshi na raia.

Msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito nchini Ethiopia alisema kuwa tume ya usuluhishi kutoka Ethiopia inapaswa kuchunguza nakala yake baada ya kupendekeza mpango wa taasisi za mpito.

Muungano wa viongozi wa waandamanaji wameitisha maandamano ya nchi nzima Juni 30 mwaka huu kushinikiza wanajeshi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.