Pata taarifa kuu
SUDANI-ETHIOPIA-USULUHISHI

Sudan: Jeshi lafutilia mbali pendekezo la Ethiopia la kuondokana na mgogoro

Msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito nchini Ethiopia amesema kuwa tume ya usuluhishi kutoka Ethiopia inapaswa kuchunguza nakala yake baada ya kupendekeza mpango wa taasisi za mpito.

Msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito Shams-Eddin Kabashi katika ikulu ya rais, Khartoum, Juni 23, 2019.
Msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito Shams-Eddin Kabashi katika ikulu ya rais, Khartoum, Juni 23, 2019. © Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya sasa ya kijeshi ya Khartoum imefutilia mbali bila kupinga pendekezo la Ethiopia. Pendekezo hilo ambalo lilikubaliwa siku ya Jumamosi na upinzani, linataka kuwepo na baraza la mpito la watu kumi na tano, likiongozwa na idadi kubwa ya raia na na kuwepo na mfumo wa kupishana kwenye uongozi wa nchi kati ya jeshi na raia.

Siku ya Jumapili, msemaji wa Jeshi Luteni Jenerali Shams-Eddin Kabashi alisema tu kwamba pendekezo hilo la Ethiopia halikuhusiana na kile kilichojadiliwa, bila kutoa maelezo zaidi.

"Tumemwambia rais wetu na makamu wa rais kwamba tumepokea pendekezo la Ethiopia na kwamba ni tofauti na yale waliyokubaliana na tume ya usuluhishi na Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Hatuwezi kuzingatia pendekezo hili mpaka pale tutakapopata majibu yaliyo wazi kuhusu kwa nini kuna tofauti, "ameonya.Msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito.

Msemaji wa Barazala la Jeshi la Mpito amesema kuwa mpango wa Ethiopia ni "tofauti" na mpango mwingine uliotolewa na Umoja wa Afrika na kuomba tume hizo mbili za wasuluhishi kurudi na mpango mmoja.

Khartoum haijakataa au kuopinga mpango huo, lakini inaonekana kuwa inataka kupoteza muda, mmoja wa waangalizi amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.