Pata taarifa kuu
KENYA-DRC-USHIRIKIANO

Kenyatta aahidi kusaidia DRC kurejea katika hali ya utulivu

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema nchi yake iko tayari kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa umma wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama sehemu ya kuhakikisha anasaidia taifa hilo kurejea katika hali ya utulivu.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga (kushoto) na rais wa DRC Felix Tshisekedi, Nairobi, Februari 6, 2019.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga (kushoto) na rais wa DRC Felix Tshisekedi, Nairobi, Februari 6, 2019. STR / Raila Odinga Press Office / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta ametoa kauli hii saa chache tu baada ya kukutana na rais mpya wa DRC, Felix Tshisekedi Tshilombo, ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza kabisa nje ya DRC tangu achaguliwe, ambapo tayari ametembelea Angola na hivi leo Alhamisi mchana anatarajia kuzuru Congo Brazzaville.

Akiwa Nairobi, Tshisekedi amekutana pia na kinara wa upinzani Raila Odinga ambaye hivi karibuni amekuwa akifanya kazi kwa karibu na rais Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta, na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raïla Odinga, wote wawili walihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa DRC Felix Tshisekedi mwezi uliopita. Ziara hiyo ya Felix Tshisekedi nchini Kenya ni njia moja wapo ya kuwashukuru wawili hao kumuunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.