Pata taarifa kuu
DRC-LAMUKA-SIASA

Muungano wa upinzani wa Lamuka walaani wito wa chuki za kikabila dhidi ya Tshisekedi

Muungano wa vyama vya upinzani Lamuka unaoongozwa na Martin Fayulu unalaani kile ulichokiita wito wa "chuki za kikabila" uliyotolewa na "watu wasiojulikana" kando ya mkutano wake siku ya Jumamosi mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wafuasi wa Martin Fayulu katika mkutano uliofanyika  kwenye eneo la Sainte-Thérèse N'Djili, Kinshasa, Februari 3, 2019.
Wafuasi wa Martin Fayulu katika mkutano uliofanyika kwenye eneo la Sainte-Thérèse N'Djili, Kinshasa, Februari 3, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo ulioitikiwa na maelfu ya watu, kuna watu waliojitokeza na kuimba nyimbo za chuki dhidi ya jamii ya rais mpya, Felix Tshisekedi.

"Muluba zua ye Boma ye" (Muluba, mchukuwe na muue), waliimba watu hao kando na eneo kulikokuwa kukifanyika mkurano wa Lamuka, kulingana na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

"Muungano wa vyama vya upinzani Lamuka haukufurahishwa na tabia ya baadhi ya watu wasiojulikana walitoa kauli za kuchochea chuki za kikabila kando ya mkutano wake wa tarehe 2 Februari," Mratibu wa muungano huo, Fidele Babala, ameandika katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.