Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-USALAMA

Askari 3 wa Ufaransa wauawa kaskazini mwa Mali

Wanajeshi wengine wawili wa Ufaransa wamefariki Jumatano hii Aprili 13, baada ya mwezao kufariki siku moja kabla.

Des soldats de l'opération Barkhane dans le centre de Gao.
Des soldats de l'opération Barkhane dans le centre de Gao. RFI/David Baché
Matangazo ya kibiashara

Gari la askari hawa lililipuliwa Jumanne hii na bomu lililokua limetegwa ardhini kaskazini mwa Mali, ambako Ufaransa imeingilia kijeshi tangu mwanzoni mwa mwaka 2013. Heshima ya kitaifa kwa askari hao watatu itatolewa wiki ijayo na Rais Hollande, Ikulu ya Elysée imetangaza.

Mabomu ya ardhini ni moja ya hatari kuu inayowakabili askari wa Ufaransa nchini Mali.

Tangu mwezi Agosti 2015, magari kadhaa ya jeshi la Ufaransa yamelipuliwa na mabomu ya ardhini au vifaa vya kulipuka viliotengenezwa kienyeji.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Mali, ambapo idadi hii imethibitishwa kwa sehemu moja na uongozi wa majeshi ya Ufaransa, gari moja ya kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa (Barkhane) lililipuliwa na bomu la ardhini tarehe 25 Machi karibu na mji wa Gao; gari jingine, lilikabiliwa na hali hiyo Februari 14 katika mji wa Kidal, na kuwajeruhi watu waliokuwemo; na miezi michache kabla, wanajeshi wa vikosi maalum (VPS) waliokua wakipiga doria walilipuliwa na bomu la ardhini katika mji huo wa Kidal, na kusababisha kifo cha afisa wa kikosi cha COS, ambapo mwili wake ulirejeshwa nchini Ufaransa.

Katika eneo lolote la operesheni la kikosi cha Barkhane, kaskazini mwa Mali ni eneo hatari zaidi. Jumanne, Aprili 12, askari hao watatu waliuawa baada ya gari lao kulipuliwa na bomu la kutegwa ardhini, ikiwa ni pigo kubwa kwa Ufaransa tangu kikosi cha Serval kuhitimisha shughuli zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.