Pata taarifa kuu
MALI-UE-SHAMBULIO

Mali: shambulio dhidi ya ujumbe wa kijeshi wa EU Bamako

Hoteli moja mjini Bamako wanakoishi wanajeshi wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya ambao unatoa mafunzo kwa jeshi la Mali ililengwa na shambulio Jumatatu jioni. Hakuna hasara iliyotokea. Shambulio hilo lilizimwa na mmoja wa washambuliaji aliuawa.

Polisi wa Mali katika eneo la hoteli iliombuliwa Bamako, Jumatatu, Machi 21, 2016.
Polisi wa Mali katika eneo la hoteli iliombuliwa Bamako, Jumatatu, Machi 21, 2016. © REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Jinsi shambulizi lilivyoendeshwa

Shambulizi liliyofanyika katika kata ya ACI 2000 ya mji mkuu wa Mali ambapo kunapatikana hoteli unakoishi Ujumbe wa kijeshi wa Umoja wa Ulaya. Inasemekana, watu wenye silaha walifanya hatua ya kwanza ya kudhibiti ndani ya kata hiyo nzuri inayolindwa vya kutosha, ambayo inapatokana karibu na hoteli Radisson Blu iliyoshambuliwa na wanajihadi tarehe 20 Novemba 2015.

Kisha waliingia katika mtaa unaoelekea kwenye hoteli ya Kaskazini-Kusini. Lakini kwenye kituo cha pili cha ukaguzi, sehemu ya kuingilia katika makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaotoa mafunzo kwa jeshi la Mali (EUTM), walirudishwa nyuma. Ilikua saa 6:40 jioni. Washambuliaji walirusha risasi, lakini askari wanaolinda hoteli hiyo walijibu haraka. Makabiliano hayo yalidumu zaidi ya saa moja na nusu.

Ni akina nani waliingilia kati?

Kwenye eneo hilo, vikosi vya usalama vya Mali vilitumwa haraka na kwa idadi kubwa : kikosi cha kupambana na uhalifu, polisi na kikosi cha ulinzi wa taifa. Umoja wa Mataifa nchini Mali kwa upande ulituma watu na magari ya kivita. Kata hiyo ilizingirwa na mpaka sasa hali imedhibitiwa.

Je, kuna washambuliaji waliofaulu kutimka?

Mmoja wa washambuliaji aliuawa papo hapo katika mapigano hayo. Alikua na silaha ya kivita na mfuko mkubwa ambao vikosi vya usalama vinaufanyia uchunguzi. Ni inawezekana kuwa ni vilipuzi. Lakini washambuliaji walikuwa angalau wawili, labda watatu, kwa mujibu wa Waziri wa Usalama wa Mali. Idadi bado inatofautiana. Mshambuliaji mwengine alijeruhiwa kwa risasi lakini alifaulu kukimbia. Askari polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL, waliokuja kusaidia, walirusha ndege isio na rubani ili kujaribu kumpata. Lakini kwa sasa, utafiti au uchunguzi haujaonyesha chochote.

Watuhumiwa wawili wakamatwa na wamekuwa wakihojiwa, lakini hakuna mtu anaejua iwapo wana uhusiano na shambulio hilo. Usiku wa Jumatatu hadi Jumanne, idadi kubwa ya vikosi vya usalam iliongezwa katika mji mkuu wa Mali.

Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hili. Utambulisho na nia ya washambuliaji haijulikani. Mamlaka ya Mali na wanadiplomasia wa kigeni wanazungumzia tukio hilo kama "kitendo cha kigaidi". Inasubiriwa madai hayo yathibitishwe na uchunguzi unaoendelea.

Usiku wa kuamkia Jumanne hii, waziri wa Usalama amesema watu hao wenye silaha walikua wakilenga labda benki ilio jirani ya hoteli ya Kaskazini-Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.