Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI

Askari wa Ufaransa auawa Mali

Askari wa Ufaransa ameuawa Jumanne hii kaskazini mwa Mali, ambako Ufaransa imekua imeingilia tangu mwaka 2013. Ni mlipuko wa bomu lililotegwa ardhini ndio umesababisha ajali hiyo mbaya.

Gari la kijeshi la askari wa Ufaransa alieuawa katika mlipuko wa bomu nchni Mali linafanana na hili (picha).
Gari la kijeshi la askari wa Ufaransa alieuawa katika mlipuko wa bomu nchni Mali linafanana na hili (picha). AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari huyo wa Ufaransa wa kikosi cha 511 amefariki Jumanne hii nchini Mali katika mlipuko wa bomu lililotegwa ardhini dhidi ya gari lake la kivita. Askari wengine wengi wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

"Heshima kubwa kwa kujitolea kwa askari aliyepoteza maisha"

Rais François Hollande ameelezea " heshima yake kubwa kwa ajili ya kujitolea kwa askari huyu kijana" na ametoa rambirambi zake kwa familia ya askari na jamaa zake.

Waziri Mkuu Manuel Valls pia ameonyesha "maskitiko yake".

Ikulu ya Elysée imetoa heshima kwa "ujasiri" wa askari Ufaransa

Katika tangazo linaloeleza taarifa hii ya huzuni, Ikulu ya Elysée imeandika: "Rais wa Jamhuri anakaribisha ujasiri na mshikamano wa askari wa Ufaransa ambao wanaendelea na kazi yao sambamba na jeshi la Mali na vikosi vya Umoja wa Matiafa kwa kuhakikisha uhuru wa Mali na kukabiliana na makundi ya kigaidi yenye silaha ambao ni tishio kwa nchi zote za Sahel. "

Eneo la kaskazini mwa Mali lilianguka mikononi mwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu wenye silaha mwezi Machi hadi Aprili 2012. Makundi haya kwa kiasi kikubwa yalitimuliwa na operesheni ya vikosi vya kimataifa vya wanajeshi iliyoanzishwa kwa juhudi za Ufaransa mwezi Januari 2013, operesheni ambayo bado inaendelea.

Lakini maeneo yote bado hayadhibitiwa na majeshi ya Mali na yale ya kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.