Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-MAPIGANO-USALAMA

Uturuki yaendelea na mashambulizi Syria

Jeshi la Uturuki na washirika wake wa Kiarabu wa Syria wametekeleza mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Syria katika ngome za wanamgambo wa Kikurdi, ambao wamewahimiza watu kuchukua silaha ili kukabiliana na mashambulizi hay

Majeshi ya Uturuki kaskazini mashariki mwa Afrin, Syria, Januari 23, 2018.
Majeshi ya Uturuki kaskazini mashariki mwa Afrin, Syria, Januari 23, 2018. REUTERS/Khalil Ashawi
Matangazo ya kibiashara

Duru za shirika la haki za binadamu nchini Syria zimesema mashambulizi kadhaa ya kijeshi yametelezwa jana jumanne katika ngome za kikosi cha ulinzi wa wakurdi. YPG katika eneo la Afrine, wanamgambo wa Kikurdi ambao serikali ya Ankara inawachukulia kama magaidi wakati serikali ya Washington ikiwapa msaada.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean Yves Ledrian, amesema baada ya vita dhidi ya kundi la Daesh, huenda mzozo ukachukuwa sura nyingine kama inavyoshuhudiwa kwa sasa katika mashambulizi ya jeshi la Uturuki nchini Syria.

Hayo yanajiri wakati huu serikali ya Urusi ikiendelea kukanusha kuhusika kwake katika matumizi ya bomu zenye kemikali nchini Syiria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.