Maporomoko yaua watu wengi Kaskazini Magharibi mwa Burundi
Watu zaidi ya 20 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na maporomoko ya mlima yaliyoangukia makazi ya watu katika kijiji cha Nyabundu, tarafani Mugina mkoani Cibitoke Kaskazini Magharibi mwa Burundi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kulingana na vyombo vya habari nchini Burundi, mpaka sasa idadi ya watu waliofariki kufuatia maporomoko hayo haijajulikana bado.
Redio Isanganiro imeripoti kuwa watu 24 wamefariki dunia kufuatia maporomoko hayo.
Lakini msemaji wa Wizara ya Usalama Pierre Nkurikiye, amesema hajapata ipoti rasmi ya vilivyoharibiwa na maporomoko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Taarifa kutoka eneo la Nyabundu zinasema mvua nyingi zilizonyesha usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi zilisababisha maporomoko ya ardhi na kumomonyoka kwa mlima mmoja ulio katika eneo hilo.