Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-USALAMA

Tume huru ya uchunguzi kuhusu Burundi yashtumu Imbonerakure

Tume huru ya uchunguzi kuhusu Burundi inayoongozwa na Doudou Diène kutoka Senegal imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

Mjini Bujumbura, mbele ya ofisi ndogo ya chama tawala cha CNDD-FDD, ambapo vijana kutoka chama hicho kuwa wanatajwa naTume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuwa ni wanamgambo.
Mjini Bujumbura, mbele ya ofisi ndogo ya chama tawala cha CNDD-FDD, ambapo vijana kutoka chama hicho kuwa wanatajwa naTume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuwa ni wanamgambo. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Burundi inaendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa miaka mitatu sasa, baada tu ya ras Pierre Nkurunziza kuchukua hatua ya kuwania muhula watatu mnamo mwaka 2015.

Tume hiyo ilieleza wasiwasi wake Jumatano hii Juni 27, ilipokua ikiwasilisha ripoti yake kwa Baraza la Haki za Binadamu miezi mitatu kabla ya kutamatika kwa muda wake. Pia tume hiyo imenyooshea kidole cha lawama vuguvugu la vijana wa chama tawala CNDD-FDD, Imbonerakure, kuhusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji, vitisho, mateso na mauaji dhidi ya wanasiasa na wafuasi wa upinzani. Serikali ya Bujumbura imefutilia mbali ripoti hiyo, na kubaini kwamba "haina ukweli wowote."

Tume hii ya Umoja wa Mataifa haikuweza kuruhusiwa na seikali ya Burundi kutekeleza kazi yake nchini humo. Lakini Mwenyekiti wa tume hiyo, Doudou Diène, anahakikisha kuwa licha ya yote hayo, waliweza kuhoji zaidi ya waathirika 380 wa vitendo hivyo kutoka Burundi au mashahidi (raia wa Burundi) walio uhamishoni na wale walio ndani ya nchi, katika miezi mitatu iliyopita.

Ushuhuda wote huu uliruhusu tume huru ya uchunguzi kuweka wazi vitendo viovu vinavyotekelezwa na Imbonerakure, vuguvugu la vijana wa chama tawala ambao Umoja wa Mataifa unawaita wanamgambo, katika kile kinachotajwa kuwa "chombo muhimu kilichowekwa kwa minajili ya kuwakandamiza wapinzani " tangu mwaka 2015. "Imbonerakure wanaizingira nchi ya Burundi, wanatoa taarifa kwa idara mbalimbali za serikali kuhusu kuwepo kwa wapinzani halisi au wa msimamo wa wastani katika kila eneo wanadhibiti kila eneo na wanawanyia vitisho raia, na kuwanyanyasa,", amesema Asuagbo Lucy, mmoja wa wamaafisa wa uchunguzi wa tume hiyo.Imbonerakure pia wanashutumiwa kufanya kazi ya polisi kinyume cha sheria, kulazimisha vijana wengine kuingizwa katika vuguvugu hilo au kuwalazimisha watu kuchangia katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.