Pata taarifa kuu
ZANZIBAR-TANZANIA

Rais wa kwanza wa Zanzibar akumbukwa leo

Watanzania wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 45 baaa ya kifo cha rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume fr/photos
Matangazo ya kibiashara

Ni siku ya mapumziko nchini humo.  

Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905  na alifariki dunia siku kama ya leo mwaka 1972 kwa kupigwa risasi.

Atakumbukwa kuongoza Zanzibar baada ya mapinduzi, ya kumwangusha Sultan mwenye asili ya kiarabu aliyekuwa akitawala kisiwa hicho kufikia mwaka 1964

Baada ya miezi mitatu ya mapinduzi hayo, Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Abeid Amani Karume anasalia kukumbukwa kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo Mwafrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.