Pata taarifa kuu
IRAN

Ulinzi waimarishwa Tehran kufuatia mkutano mkuu wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote

Zaidi ya askari laki moja wametawanywa maeneo mbalimbali nchini Iran hususan katika mji mkuu wa Tehran kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika kipindi chote cha mkutano wa dunia wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote wenye lengo la kupambana na dunia ya silaha ya Nuklia.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Ban Ki Moon ni miongoni mwa washiriki wa mkutano wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote unaofanyikia Tehran  Iran
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Ban Ki Moon ni miongoni mwa washiriki wa mkutano wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote unaofanyikia Tehran Iran israelmatzav.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Naye kiongozi mkuu wa jeshi la mapinduzi Generali Mohammad Ali Jafari amenukuliwa akisema kwa uwezo wa Mungu anaamini kufanyika kwa mkutano huo kutaweka alama ya ushindi kwa Iran kufuatia mvutano wa vyombo vya habari baina yao na mataifa ya magharibi.

Iran imefungua mkutano wa Dunia wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote ikitoa ombi lao kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupambana na dunia ya Silaha za Nuklia, ingawa nchi hiyo imekuwa ikishukiwa na nchi za magharibi kuwa imekuwa ikitengeneza mabomu ya atomiki.

Iran inatumia mkutano huu kutoa changamoto kwa mataifa ya magharibi na washirika wake, ambapo mkutano huu utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na waziri mkuu wa India Manmohan Singh ambae nchi yake imeendelea kuwa mteja mkubwa wa Mafuta ya nchini Iran wakati huu Iran ikipambana na vikwazo kufuatia mpango wake wa Nuklia.

Hali kadhalika Iran imesema kuwa inapanga kutoa mapendekezo ya kumaliza mapigano nchini Syria, hata hivyo hakuna makundi ya waasi kutoka Syria yatakayohudhuria mkutano huo kwa kuwa Tehran ni mshirika wa karibu wa Utawala wa Rais Bashar Al Assad.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.