Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Usafiri wa anga waanza tena nchini Australia

Usafiri wa anga nchini Australia leo umeanza tena kufanya kazi kufuatia huduma hiyo kusitishwa kwa muda juma hili kutokana na kusambaa kwa majivu ya Volakno iliyolipuka nchini Chile katika anga la nchi hiyo na kusababisha ndege kushindwa kuruka.

Moshi wa Volkano toka katika milima ya  Eyjafjallajokull
Moshi wa Volkano toka katika milima ya Eyjafjallajokull Reuters
Matangazo ya kibiashara

Juma hili mamlaka ya naga nchini humo kupitia kwa msemaji wake ilitangaza kusitisha huduma zote za usafiri wa naga kwa muda kutokana na kuendelea kusambaa kwa kasi kwa vumbi la majivu ya Volkano inayoendelea kulipuka nchini Chile.

Licha ya huduma hiyo kuanza kutolewa katika baadhi ya vituo vya ndege, bado maelfu ya wananchi wameendelea kusota katika viwanja vingi kutokana na mashirika ya ndege zinazofanya safari zake bara la ulaya kushindwa kuruhusu ndege zao kuendelea kufanya kazi.

Maofisa wa anga nchini humo pia wameendelea kuonya kuwa huenda vumbi hilo la Volkano likaendelea kusambaa katika nchi nyingi ambapo sasa imeelezwa athari za moshi wa Volkano hiyo zimeanza kuelekea katika nchi ya New Zeland.

Hata hivyo mamlaka nchini humo zimeonya baadhi ya makumpuni yaliyoanza kurusha ndege zake hii leo, zikisema kuwa hali ya hewa huenda ikabadilika muda wowote na kutaka hatua za dharura kuchukuliwa mara moja.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.